Ijumaa, 18 Agosti 2017

KOMAMANGA .


        Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala haya,nakukaribisha tena ili kufahamu umuhimu wa tunda lingine aina ya Komamanga (POMEGRANATE kama waingereza wanavyoliita tunda hili).Ni tunda la tofauti kidogo kati ya matunda mengine ambayo tumekwisha yaona hapo awali kwani lina uwezo mkubwa sana ukilinganisha na matunda mengine,linatumika kutengenezea madawa ya aina mbalimbali ambayo hutumika katika vituo vya afya.Dawa hizo ni kama vile Tannis (punicalin na punicalagin), Flavonoids, Alkaloids, Steroids, Triterpenes na Polyphenols. Dawa hizi hupatikana katika magome, majani, mbegu, maganda ya matunda, juisi ya matunda na katika maua ya mkomamanga. Tunda la komamanga pia lina vitamini C na E kwa wingi amabazo tumeona mwanzoni kuwa na kazi kubwa kama kupambana na sumu mwilini (anti-oxidant) na kuharakisha uponaji wa vidonda (vitamin C) pamoaja na madini ya potassium na copper.

             Kihistoria tunda hili linajulikana sana na watu wa mashariki ya kati (middle east) kwani limetajwa sana katika vitabu vya dini kama tunda lenye uwezo mkubwa na lililopendwa na watu wenye hekima.Moja kati ya kazi kubwa inayofanywa na tunda hili ni pamoja na kuzuia kasi ya uzalianaji na ukuaji wa virusi vya UKIMWI,hivyo kupelekea tunda hili kuaminika kwa kupunguza kasi ya ukimwi kwa wale waathirika na ugonjwa huo.
  Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la kisayansi la BMC infectious diseases (4) 41-45(2004). Matokeo yanayofanana na hayo pia yalithibitika katika utafiti mwingine uliofanywa na Kun Silprasit na wenzake mnamo mwaka wa 2011 na kupewa jina la “Anti-HIV-1 Reverse transcriptase activities of hexane extracts from Asian Medicinal Plants”. Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la kisayansi la “Journal of Medical Plant Research Vol. 5 (17), pp. 4194-4201, 9 Sept 2011”.
   Tunda hili linaaminika kuwa na kazi nyingi ikilinganishwa na matunda mengine na limejizolea umaarufu kulingana na uwezo wake mkubwa katika kupambana na ugonjwa huu mkubwa.Tuangalie faida zingine za kiafya zitokanazo na tunda hili la Komamanga.

TUMBO KUJAA GESI
  Vyakula tunavyokula vinazalisha gesi tumboni wakati wa kusagwa kwake,vyakula vya jamii ya mikunde hasahasa.Hii hupelekea tumbo kuunguruma mara kwa mara na kujihisi kushiba muda mwingi,ingawa siyo hali ya kawaida  na watu wengi wanalichukulia jambo hili kama ni kitu cha kawaida.Tumia majani ya komamanga kwa kuyachemsha na kunywa maji yake angalau mara mbili kwa siku kila baada ya mlo wako.

KUHARA DAMU.

  Bakteria ndani ya tumbo husababisha vidonda katika ukuta wa tumbo ambavyo huchelewa sana kupona na huvujisha damu ndani kwa ndani (haemorrhage),bakteria hao ni kama vile H.Pyroli na wengineo.Kwa kuwa tunda hili lina uwezo mkubwa katika kupambana na bakteria na virusi vya aina mbali mbali ndani ya mwili wa binadamu,ukitumia kwa muda mrefu linaweza kumaliza kabisa tatizo hilo.

KUDHIBITI TINDIKALI TUMBONI.

  Mchanganyiko wa madini yanayopatikana ndani ya tunda hili huzuia hali ya asidi tumboni (neutralization) na kusababisha utulivu kama ulikua na vidonda vya tumbo.tumia juisi (angalau glasi moja) kila baada ya mlo wa mchana.

KIHARUSI/STROKE.

  Huu ni ugonjwa wa kupooza kwa mwili unaotokana na kudhohofu kwa mishipa ya damu inayolishia ubongo.Kwakuwa tunda hili lina uwezo mkubwa wa kupambana na hali yoyote ya shambulio katuka damu na tunaona kwamba visababishi vya kiharusi kama vile sukari nyingi kwenye damu ambayo husababishwa na obesity,shambulio la wadudu/bakteria katika damu,vinaweza kuzuiliwa na tunda hili la komamanga.Nakushauri pendelea kutumia tunda hili kwa manufaa mbalimbali na siyo ulitumie kwa bahati mbaya.

MAGONJWA YA NYAMA ZA MOYO.

    Madini aina ya pottasium yanayopatikana ndani ya tunda hili yana faida kubwa sana ya kuimarisha uimara wa misuli na kukufanya uwe na misuli yenye nguvu pia.Hii itakupelekea kuondokana na tatizo la kuuma kwa misuli ya moyo ambayo mara nyingi humpata mtu ambaye hafanyi mazoezi mara kwa mara na kuufanya moyo wake kuwa mdhaifu.

TATIZO LA UNENE (OBESITY).

  Kama tulivyoona hapo juu kwamba kuongezeka kwa unene yaani Obesity kunasababishwa na mambo mengi kama kuongezeka kwa sukari ndani damu.Tatizo hili linaweza kuondoshwa kwa utumiaji wa tunda hili kwani lina sukari rahisi ambayo mmengenyo wake huwa nia rahisi ikilinganishwa na sukari inayopatikana ndani ya nafaka kama mahindi na mchele.Utaona wazi katika kutatua tatizo hili pia tatizo la kisukari litakukalia mbali na maisha yako daima.

Ukijilinganisha kiafya kati ya wewe na mtumiaji wa tunda la komamanga utaona tofauti kubwa sana kati yenu,kwani baadhi ya magonjwa ambayo yanakusumbua wewe mara kwa mara mwenzako atakwambia hayajawahi kumpata huu ni mwaka wa tano au sita.Ndipo utakapogundua umuhimu wa kutumia tunda hili.
 Kuna madhara ya kutumia tunda hili kwa wingi,kwani kama tunavyojua kwamba kila kitu ukizidisha kuna madhara utakayoyapata,pia hata ukizidisha dozi ya tunda hili kuna madhara ambayo utakayoyapata na madhara hayo ni kama ifuatavyo;
               Madhara yanayoweza kutokea kwa kutumia dawa-lishe hii (Adverse reactions)
Matumizi ya kipimo kikubwa cha dawa hii ikiwa katika hali yake ya asili (zaidi ya gram 80) kinaweza kusababisha kizunguzungu, maumivu makali ya kichwa, kushindwa kufumbua macho, kutapika, kuzimia na wakati mwingine inaweza kusababisha kifo. Dawa hii pia inaweza kusababisha mwili kunyong’onyea, kutokuona vizuri, kushitukashituka kwa misuli na kutetemeka kwa mikono kama mlevi (tremors).

                                PHONE:   0673666791 
                                Email: goldamplat@gmail.com


     Kwa swali lolote kuhusiana na afya yako usisite kuuliza.
      JENGA AFYA YAKO NA AMPLAT-AFYA KWANZA

Alhamisi, 16 Februari 2017

 Amplat AFYA KWANZA.

  Ni wasaha mwingine tena tunakutana katika kuelimishana juu ya umuhimu wa baadhi ya matunda kiafya,tuanze kwa kumshukuru Mungu kwani ndiye muweza wa yote na ametujalia kuwa wazima mpaka sasa.Natumaini tunaendelea na utaratibu wa kufuata lishe sahihi za matunda ilimkujikinga na magonjwa na kuziepusha hata familia zetu,Tujipongeze kwa hilo.

       Leo nakukumbusha umuhimu wa matumizi ya matunda kulingana na vitu vyote tulivyoviona tangu tulipoanza mpaka siku ya leo ili kama umesahau ukumbuke unapaswa kufanya nini na usijione kama upo peke yako.Nashukuru kwa wale wote tuliowasiliana nao nikawaeleza kulingana na walivyohitaji na sasa wananipa matokeo sahihi wakisema kwamba hawakujua mapema uwezo mkubwa wa matunda juu ya miili yao.Hakika si dhahania matunda yana nguvu kubwa sana katika kuijenga na kuilinda miili yetu kwa aina mbali mbali dhidi ya magonjwa nyemelezi.

    Kwa wewe ambaye umetumia kulingana na maelekezo na haujaona tofauti yoyote kabla na baada ya kutumia,nikukaribishe kwa kuchukua simu yako na kuwasiliana nasi kwa namba zetu hapo chini ili tukuelekeze zaidi nini cha ziada ufanye au kama ulikosea juu ya matumizi tukuifuatilie kwa ukaribu ili kukupa maelekezo sahihi juu ya afya yako.Nina imani kwa wale wote waliotilia nia na kushughulikia swala hilim wameona matokeo yakuridhisha kwani hakuna uongo wala siasa katika kutumia matunda kama lishe bora.Tunda la kulainisha ngozi (parachichi),litalainisha ngozi na tunda la kuondoa sumu (tango) litaondoa sumu na sio siasa,hivyo basi nikutoe hofun wewe ambaya umetumia dawa lishe ya matunda na haujaona tofauti.

  Amplat AFYA KWANZA ipo kwaajili ya kukupa elimu juu ya umuhimu wa lishe bora za matunda pamoja na kukusaidia katika kutatua matatizo yako kiafya kwa kukuunganisha na daktari unaestahili huduma zake kulingana na tatizo lako.Usiogope kuuliza pale usipoelewa ufanyaje ili upate lishe kamili ya utumiaji wa matunda sisi tupo kwaajili ya kutoa msaada.

   Ewe mama,dada,kaka,baba na watoto pia,kuwa na afya bora ni haki yako ya msingi hivyo nakushauri unapoona haupo sawa kiakili,kiafya na hata kimawazo usisite kuwasiliana nasi tutakusaidia.Kukaa kimya wakati una tatizo la afya sio vyema na waswahili husema kwamba MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA sasa basi usisubiri mpaka mauti ikufike ndipo tujue kwamba ulikua unaumwa nini.Mara tu uonapo hali ambayo si ya kawaida mwilini mwako usisite kutujulisha nasi tutakusaidia...Ahsante

PHONE:  0673666791

Email:     Goldamplat@gmail.com

Jumanne, 7 Februari 2017

PERA



     Ni wakati mwingine ndugu mpenzi mfuatiliaji wa makala haya tunakutana tena kuelekezana kuhusu faida za lishe ya matunda mbalimbali.Leo tutaangalia umuhimu wa tunda la aina ya pera kwani wengi wamekua wakiniuliza kuhusiana na faida za tunda hili hata kabla sijachukua maamuzi ya kuliandika na kulitolea ufafanuzi
 Kwanza tuanze kumshukuru mungu kwa yote aliyotutendea na kutufikisha hapa tulipo kwa siku ya leo,kama ni mgonjwa unapaswa kumshukuru mungu pia na kutafuta njia gani ufanye ili uondokane na ugonjwa huo.Twende pamoja katika kuangalia faioda mbali mbali za tunda hili;

 Kama tunavyolifahamu tunda la pera ni tunda ambalo watu wengi hawapendi kulila kawaida kwani lina mbbegu ambazo ni ngumu sana ambazo hata watoto wadogo hawawezi kuhimili kuzitafuna.Kuna pera la kijani,njano na jekundu yote haya ni sahihi kuliwa lakini yanaonyesha hatua za ukomavu wake,lakini kwa pera la kijani mara nyingi huwa linakua bado bichi hivyo ukila pera hilo utasumbuliwa na tumbo kwani virutubisha vyake huwa bado havijakamilika.
     Licha ya kuwa na sifa hiyo hakumaanishi eti usle kabisa tunda hili hapana,unaweza ukalisaga na kutengeneza juisi ambayo itakufanya upate virutubisho vile vile ambavyo ungevipata kwa kulila likiwa lenyewe.Pera kama yaaalivyo matunda meeengine lina faida mbali mbali kama vile;

VITAMINI C
 Tumeona tangia mwanzo faida za vitamini C kwenye mwili wa binadamu na kama utakumbuka vizuri ni karibia kila aina ya tunda lina kirutubisho hiki hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kwamba matunda ni chanzo kikubwa cha vitamini C.Kazi kubwa ya kirutubisho hiki ni pamoja na kuzuia magonjwa ya fizi na taya (Kiseyeye) hasahasa kwa watoto wadogo.Mpe mwanao kirutubisho hiki kwa kumkinga dhidi ya ugonjwa huu.Tunda la pera lina 120mg za vitamini C ambayo kwa mwanaume ni 90mg huhitajika kila siku na 75mg ambazo huhitajika kwa mwanamke.Faida nyingine ya kirutubisho hiki ni pamoja na kusaidia katika utengenezaji wa tishu mpya mwilini na kuchochea ufyonzaji wa chakula kilicho sagwa vyema mwilini,kwa kutokula pera na kukosa vitu hivi utaona ni kwa kiasi gani unakosa vitu muhimu.

MATATIZO YA UZAZI KWA WANAWAKE.
 Kuna kirutubisho kimoja aina ya FOLATE ambacho hupatikana ndani ya tunda hili la pera kinachofanya mayai ya mwanamke kukua vyema.Licha ya kuwa na tatizo la homoni za uzazi mwilini mwa mwanamke,anaweza kukabiliana na tatizo hilo kwa kutumia tunda la pera kama dawa ya tatizo lake na matokeo atayapata.Kwa dada mwenye matatizo ya uzazi kama kushindwa kuona siku zake na hata yule anayeshindwa kubeba mimba,kuna siri kubwa imefichika katika matumizi ya matunda siyo pera tuu bali hata na matunda mengine.kirutubisho hicho kina kazi nyingi zihusianazo na uzazi hivyo unaombwa kutumia tunda hilo kwaajili ya kuondokana na matatizo yasiyo ya lazima.

HUPUMZISHA MWILI.
 Uwepo wa vitamini B3 na B6 kunafanya mwili kuwa mtulivu na wenye mwendokasi uliotulia zaidi.Nakushauri baada ya kazi na uchovu wa mwili kula pera kwa ajili ya kuuburudisha mwili na kukufanya utulie kwa utulivu sahihi.Watafiti wanadai kuwa pera huuupa ubongo afya njema na mtulizo wa akili ulio sahihi na kuwa kufanya hivi huongeza uwezo wa utendaji kazi wa akili ya mtu,ukimwanzishia mwanao leo hii lishe sahihi ya tunda hili utamfanya kuwa na akili njema na ukuaji wake utasawijika kwani ni ubongo huo huo unaoooooorekebisha masuala ya ukuaji.

MATATIZO YA CHOO.
 Kamba lishe zilizopo ndani ya tunda hili zina mchango mkubwa sana katika kurekebisha matatizo ya choo,kwa wale wote wanaopata choo kigumu wanaweza wakaanza kutumia mapera kama njia mbadala ya kutibu tatizo lao.Pia kama una kumbukumbu nzuri utaona kwenye kila aina ya tunda tuliloliona mwanzo lina mchango mkubwa sana wa suala kama hili hivyo yunaweza kusema kwamba matunda yanatusaidia sana kukabiliana na tatizo hili.Kazi kubwa ya kambalishe hizi ni kusaidia usagaji wa chakula mwilini na ufyonzwaji wa maji katika sehemu ya mwisho ya usagaji yaani kwenye utumbo mkubwa.

DAWA YA TUMBO.
 Hapa ifahamike wazi kwamba majani ya mti wa mpera yana mchango mkubwa sana katika kutibu tumbo lolote lile liwe la kuhara au kuuma kwa kawaida.Sio dawa yenye masharti wala haikuhitaji kulipia hata gharama zaidi ya muda wako tuu,unashauriwa kuchukua majani machanga ya mpera na unaweza ukayatafuna bada ya kuyaosha au ukayachemsha kwa muda wa dakika kumi na ukanywa maji yake hayo kwa kipimo sahihi (usisubiri yapoe).

MZUNGUKO WA DAMU.
 Kutokana na kiasi kikubwa cha madini ya mangenese na iron iliyopo ndani ya tunda hili ni mchango mkubwa katika utengenezaji wa damu kwani madini ya chuma ndiyo hasa yanahitajika kwaajili ya kutengeneza damu.Uwepo wa madini haya mwilini kutokana na ulaji wa mapera utakuwezesha kukufanya uwe na utajiri mwingi wa damu na kuondoa matatizo yote yatokanayo na upungufu wa damu.
Pera pia lina kiasi kikubwa sana cha FOLIC acid ambayo ndiyo hitaji kuu la utengenezwaji wa damu ukitilia ndani madini ya iron.Asidi hii husaidia kuzuia ugonjwa wa anaemia kwani ndio ugonjwa mmojawapo utokanao na uchache wa damu mwilini.

  Antioxidant (kiondoa sumu) kilichomo ndani ya pera kina kazi muhimu san aya kutibu na kuondoa bacteria wasiohitajika tumboni,baadhi ya bacteria waliopo tumboni huzaliana kwa wingi na kusababisha hata UTI kwa wanawake.Si hayo tuu bali na magonjwa mengi kama kichwa kuuma,miguu na hata kuhara pia huondolewa kwa ulaji wa tunda hili,chukua maamuzi sahihi kama unaijali afya yako sasa.
   Anza sasa na usisubiri kwa ni bado hujachelewa,fuata kanuni sahihi za lishe ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya lazima uwe na afya bora.
Kwa maelezo,maswali na ushauri kuhusiana na afya yako usisite kuwasiliana nasi kwani tupo kwaajili ya kukufahamisha na kuhakikisha tuna share kile tunachokijua nawe pia ufaidike...Ahsante

PHONE: 0673666791

Email: goldamplat@gmail.com

Ijumaa, 3 Februari 2017

APPLE (TUFAA)

    Habari za muda huu ndugu mfuatiliaji wa makala haya,ni matumaini yangu u mzima wa afya na kama una matatizo ya kiafya,kiroho na hata mengine yatofautianayo na hayo ni wakati wako kumgeukia mungu na kumuomba akupe njia ya kuweza kukabiliana nayo.

Leo nimewiwa kukuletea matumizi sahii ya matunda katika afya zetu dhidi ya kujikinga na kupambana na magonjwa mbalimbali na tutaangalia umuhimu wa tunda aina ya apple (tufaa).Je unakumbuka ile kauli ya APPLE EATING KEEPS AWAY FROM DOCTOR? Basi kama hukumbuki basi ndivyo ilivyo na ni kweli kutokana na kazi nzuri zifanywazo nz tunda hili.

    Matufaa yana Vitamini K,nyuzinyuzi za chakula pamoja na dawa-lishe (phytochemicals) aina ya quercetin flavonoid hivyo kukuwezesha kupata virutubisho sahihi vinavyohitajika na mwili wako.matatizo mengi huondolewa na tunda hili na kukufanya uwe na mwili mwepesi pamoja ana afya njema kama utafuata taratibu za lishe katika matunda haya.Tuangalie faida zake kiafya;

HUREKEBISHA AFYA YA MAPAFU.
 Katika matunda ambayo yana mchango mkubwa juu ya magonjwa na matatizo ya mapafu ni pamoja na tunda hili,umaarufu wake umetokana na kazi kubwa ya kurekebisha maswala ya mapafu.Majimaji yaliyopo kwenye apple yana mchango mkubwa sana juu ya kuondoa bakteria ambao wanavamia mapafu na kuleta magonjwa kama kifua kikavu.
Kuna asilimia kubwa kwa apple kutibu kansa ya mapafu kutokana na kazi za kuzuia maambukizi ndani ya mapafu,wataalamu wengi wameshauri kula tunda hili kwa lengo la kurekebisha afya yako ya mwili mzima kiujumla.

HUZUIA MAWE KWENYE FIGO.
 Kwa kurekebisha mzungoko mzuri wa damu mwilini,apple linauwezo mkubwa wa kusafisha damu yako na kufanya ini pampja na figo kupunguziwa kazi ya kuchuja taka mwili ndani ya mwili.Magonjwa ya ini na figo huzuiliwa kwa tunda hili la apple.

SOLIDI YA TUMBO (COLITIS).
 Kama unasumbuliwa na tumbo la kuhara na hujisikii vizurim kila baada ya kula unashauriwa kuanza mara moja kutumia tunda hili kama kinga kwani linasaidia katika kurekebisha udhaifu wowote wa tumbo.
Ulaji wa apple unatia nguvu mwili na kukufanya kukaa muda mrefu bila kusika njaa au uchovu.Ma apple matatu yanakufanya kukaa masaa nane pasipo kuhisi uchovu mwilini mwako na kukuweka active kwa muda wote huo.

MAGONJWA YA KUHARISHA.
 Hii huonekana katika mambo yote mawili kwenye kuharisha au kupata choo kigumu nyuzi nyuzi zilizopo ndani ya tunda hili kama kwenye matunda mengine tuliyoyaona hapo awali,zitakufanya uondokane na tatizo kama hili.
Tumia kwa lengo la afya na sio kwa mazoea kama kusitisha matumizi au kula ukijisikia kufanya hivyo kwani hutaona manufaa yoyote na utaishia kulalamika kwamba hujapata matokeo mazuri.

MATATIZO YA DAMU.
 Matatizo kama blood pressure na anaemia hurekebishwa kwa ulaji wa matunda haya kwani lina kiwangi kikubwa cha calcium 10mg ambacho huweka sawa uwiano wa minerals zipatikanazo ndani ya damu.hupunguza kiasi cha Nacl ambacho hutofautisha na kufanya pressure ipande kwa kiasi kikubwa katika damu na kurudisha uwiano sawa 
 Kwa uwingi wa iron na arsenic pamoja na phosphorus husaidia kuongeza madini muhimu katika kurekebisha damu yako mwilini.

NB: Ulaji wa apple moja kwa siku ni zaidi ya mtu aliyekula mikate mitano isiyotiwa amira.

  Ulaji wa matunda haya kila siku utakufanya umsahau daktari na kukuweka mbali na hospitali,pia utamsababishia daktari kukosa ajira yake.
Nakushauri kuanza leo kutmia tiba hizi ili iwepo tofauti kati yako wewe na mtu ambaye alipuuzia ili apate mfano kwako jinsi ya afya yako itakavyokua bora.
Usisite kuwasiliana nasi muda na saa yoyote kama uan swali au maoni yoyote kuhusiana na afya yako...Ahsante

PHONE:  0673666791

Email: goldamplat@gmail.com

Jumatano, 1 Februari 2017

ZAITUNI.


   U hali gani ndugu msomaji wa makala haya ya AFYA KWANZA,ni matumaini yangu uko poa na mwenye afya njema tunapaswa kwa pamoja kumshukuru mungu kwa kutufanikishia jambo hilo.

     Leo tena ni siku nyingine ambayo tutaeleweshana kuhusu mambo fulani yahusuyo afya zetu kutokana na ulaji wa tunda aina ya zaituni.Tunda hili linaweza lisijulikane na wengi miongoni mwetu kwani linaoatikana kwa asilimia ndogo nchini ketu lakini limeonekana kuwa na kazi nyingi muhimu katika miili yetu.Tuangalie baadhi ya kazi zake hizo ni kama ifuatavyo:

HUPUNGUZA UZITO
 Tunda la zaituni limekua likiorodheshwa sana kwenye lishe za kupunguza uzito/unene,hii ni kutokana na ukweli kwamba tunda hili lina mafuta (olive oil) mepesi ambayo hayawezi kuganda ndani ya mwili na matumizi yake hutumika haraka baada ya kuonekana ndani ya mwili.Kwa watu wenye uzito uliopitiliza niwashauri kuanza kutumia tunda hili.

KUONGEZA NGUVU ZA KIUME.
 Kutokana na kurekebisha afya ya damu mwilini na kukupa nguvu ya mzunguko mpya mwilini,hamu na uwezo wa kimapenzi huongezeka ndani ya mwili wa mtumiaji wa tunda hili.Kutokana na uwezo huo watu wamekua wakilisifia tunda hilo kwa kazi yake hiyo kubwa bila kujua linafanya nini kukamilisha kazi hiyo.

TATIZO LA MAFUA.
 Wengine hutumia mafuta ya mizeituni (olive oil) kupaka kwenye upeo wa eneo la mbele ya pua kama dawa ya kutibu ugonjwa wa mafua,lakini mpaka sasa bado haijafahamika wazi ni kwanini mafuta haya hutibu mafua kwa dizaini kama hiyo ya VIKS-KINGO.

MAGONJWA YA NGOZI.
Hii ni kweli na inasaidia kwa kiasi kikubwa sana kwa mtumiaji kwani tunda la zaituni lina kiwango kikubwa sana cha vitamin D ambayo ndiyo hasa hutumika katika kurekebisha matatizo ya ngozi.Paka mafuta ya mizeituni na utaona tofauti ndani ya muda mchache

HUREKEBISHA TATIZO LA NYWELE.
 Kwa wale wenye nywele za kukatika na zilizojikunja,unaweza kutumia mafuta haya kwa kuzirefusha na kuzuia zisijikunje tena,vitamini D iliyopo ndani ya tunda hili husaidia kwa kiasi kikubwa kurekebisha afya ya ngozi kwenye kichwa ambayo huruhusu ukuaji mzuri wa mizizi ya nywele.Unaweza kuona wazi kwamba mafuta mazuri ya nywele ni OLIVE OIL.
            NB: Isionekane kama nafanya promotion ya baadhi ya mafuta ya nywele na vipodozi,Hapana.

HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KANSA
Mafuta ya zeituni (olive oil) yana olecanthal na of mimics inayozalisha ibuprofen inayosaidia  kupunguza hatari ya kupata cancer.Ni mafuta mazuri kwa yule atakaye jali afya ya mwili wake na kuitetea na ifahamike wazi kwamba wapo wagonjwa wa kansa ambao wanatumia mafuta ya mizeituni katika mlo wao wa kila siku kama kupunguza /kufisha sumu ya kansa mwilini.

NI DAWA SAHIHI YA UBONGO.
 Hii ni kwa watoto wadogo ambao wanakua,virutubisho vipatikanavyo kwenye mafuta ya tunda hili likiwa bado halijapikwa ni muhimu sana ukilinganisha na vile ambavyo hupatikana baada ya kuyapika mafuta hayo.Muanzishie mwanao utaratibu wa kumnywesha mafuta mabichi ya mzeituni ili kulinda afya yake na kumfanya awe mchangamfu na mwenye akili timamu.

DAWA YA MASIKIO KWA WATOTO WADOGO.
 Watoto wenye matatizo ya masikio kama kuwashwa mara kwa mara na kutokwa na uchafu mwingi mwilini wnaweza wakaondokana na tatizo hilo kwa kumuanzishia dozi ya mafuta hayo.Matone mawili mpaka matatu mara mbili kwa siku kutafanya tatizo hili kupotea kabisa.
Ifahamike wazi kwamba mafuta ya mzeituni (olive-oil) baada ya kupikwa hupoteza ubora wake na kutengeneza sumu lishe ambazo zitatolewa nje ya mwili bila kufanya kazi yoyote.Hivyo basi ni muhimu kuanzisha utaratibu wa kutumia mafuta mabichi ya mizeituni kuliko kuya[pika kwanza.

Kwa ushauri na maswali kuhusiana na tatizo lolote linanalo kusibu,usisite kuwasiliana nasi kwa namba hizo apo chini,,,,,Ahsante.

         Pia kuna matumizi ya kiimani kuhusiana na mafuta yatokanayo na matunda haya.
    NB: Ikumbukwe kwamba hatutolei mafunzo ya afya kwanza kutokana na imani ya mtu fulani,bali hata wasioamini nao wana haki katika jamii inayowazunguka.

                       PHONE:  0624259822

Jumatatu, 30 Januari 2017

  UKWAJU.


    Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala haya,nakukaribisha tena ili kufahamu umuhimu wa tunda lingine aina ya Ukwaju.Ni tunda la tofauti kidogo kati ya matunda mengine ambayo tumekwisha yaona hapo awali lakini leo ngoja tuangalie umuhimu wa utofauti wake na matunda mengine.

    Kidogo ni tunda la kushangaza kwani lina ladha tamu na chachu,tunda hili unapoanza kula kwanza lazima likusisimue ndipo uendano nalo na imekua ni vigumu kwa watoto wadogo kulila tunda hili wenyewe kama wenyewe kutokana na ladha yake.Ulaji wake haujatofautiana na matunda mengine kwani unaweza kulila kama tunda,ukatengeneza juisi na ukanywa na hata ukatumia kama siagi.Kusema kweli ni tunda lenye maana kubwa kutokana na kazi lilizokua nalo,tuangalie baadhi ya kazi hizo ni kama ifuatavyo.

HUTIBU HOMA.
 Kuanzia homa ya tumbo mpaka homa ya manjano tunda hili hutibu pasipo kuangalia.Hii ni kutokana na asidi liyopo ndani ya tunda hili inayozuia kabisa uzalianaji wa bacteria hatari ndani ya tumbo na kuwaacha wale wanaohitajika kubaki tuu.Imetumika kama dawa yenye manufaa zaidi kwani mtu akiumwa tumbo na kutumia ukwaju basi amejihakikishia pona yake.

HUSAIDIA USAGAJI WA CHAKULA.
 Kama yalivyo matunda mengine,ukwaju una nyuzi nyuzi ambazo husaidia katika usagaji wa chakula na kukupa choo kizuri kama tulivyoona katika matoleo ya nyuma.Kwa mwenye tatizo kama hili hatakiwi kuuliza afanye nini ili aweze kujiponya wakati dawa ya ukwaju tayari ipo na inapatikana sokoni.

HUTIBU VIDONDA.
 Vidonda vya kuungua hupona kwa kutumia ukwaju,lakini mara nyingi hutokana baada ya mchanganyiko wa tunda hili na asali.Mchanganyo utakaotumika kama dawa unatofautiana kulingana na sehemu ya jeraha au ukubwa wa jeraha pia.

HUTIBU MAAMBUKIZI YA KOO.
 Bakteria pamoja na protozoa wengine wanaoshambulia mfumo wa upumuaji huzuiwa kufanya hivyo mara tuu wanapotaka kuingia kwenye sehemu za ndani kabisa za mfumo huo kutokana na asidi inaypatikana ndani ya tunda hili,hii itakuweka huru na magonjwa yote ya koo na hata ya mfumo wa chakula kwani ni koo hilohilo ndilo linalounganisha mifumo hiyo miwili.

HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KANSA.
 Tunda la ukwaju limewasaidia wengi katika kurekebisha afya zao na kupunguza uwezekano mkubwa wa kupata kansa kwani ladha yake ya uchachu hairuhusu ukuaji wa kansa mwilini.Unashauriwa kutumia mara kwa mara ili kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata kansa mwilini mwako.Kinga za ukwaju zitazuia ukuaji wa kansa kama zitapatikana kwa wingi mwilini mwako na si vinginevyo.

UKOSEFU WA HAMU YA KULA.
 Kwa wale wanaokosa hamu ya kula chakula,tunda la ukwaju ni msaada mzuri kukurejesha katika hali yako madhubuti.Ingawa watoto wengi hukumbwa na tatizo hili pale ambapo wanakua au wamepatwa na homa,andaa juisi yako ya ukwaju na kisha tumia kikombe kimoja nusu saa kabla ya kula utaona mafanikio.

    kutokana na kazi hizo,tunashauri tunda la ukwaju lisikose katika mlo wako wa kila siku kwani lin kazi kubwa sana ukilinganisha na matunda mengine ingawa baadhi zinafanana.Tumia ukwaju kama dawa kama ninavyokwambia kwenye matunda mengine na sio utumie pale ambapo unaona tatizo limekufika kwani hata kama utapata mafanikio hayatakua makubwa kwani matunda mengi ni kinga dhidi ya magonjwa na machache ni dawa hivyo unapaswa kutumia kwa kujitaadharisha na magonjwa yajayo.

  Kama utakua unafanya hivyo kwa utaratibu wa kujiwekea ulinzi na akiba ya kinga mwilini utakua mbali kiafya na hautasumbuliwa na magonjwa nyemelezi kirahisi,lakini hakikisha unamshauri na ndugu au rafiki na hata mwenzako uliye nae jirani kufuata kanuni na taratibu za afya ili aepukane na magonjwa.
  Sina la ziada kwa siku ya leo,kwa maswali juu ya afya yako na ushauri wowote usisite kuwasiliana nasi tutakusaidia vyema kwa wakati wowote na muda wowote.Ahsante

Kwa mawasiliano usisite kututafuta;

  PHONE : 0673666791

  Email:  goldamplat@gmail.com

Alhamisi, 26 Januari 2017

ZABIBU.




     Ni matumaini yangu u mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku katika kujenga nchi yenye nguvu.Nchi imara haiwezi kuja kama wajenzi wake wana afya dhaifu itakua ni dhahania hivyo hakikisha unafuata kanuni za mlo wa afya na kinga mwilini mwako ili kupata afya iliyo thabiti.
  Leo mezani kwangu nimekuandalia tunda lingine ambalo ni moja kati ya tunda la karne na karne lenye sifa na uwezo mkubwa,nalo si lingine bali ni Zabibu.

  Katika matunda yaliyojizolea umaarufu mkubwa kuanzia karne ya sita ni tunda hili.ni la zamani sana na lilitumika kutengenezea pombe (mvinyo) tangu enzi za watu wa kale.Kusema ukweli tunda hili ni tamu na linapendwa na kila mtu hasa hasa na watoto.
  Kuna aina tatu ya zabibu nayo ni zabibu za kijani,nyekundu na kama nyeusi (dark-red),aina zote hizi huliwa kwa njia mbalimbali kama vile kwa kutengenezewa juisi,zabibu zilizo kaushwa kama raisin na kama tunda la kawaida  kama matunda mengine.Tuangalie faida kuu za tunda hili;

 VITAMINI B COMPLEX.
  Karibu aina zote za vitamini B unazozifahamu zipo humu kwenye zabibu,hii inalipa sifa tunda hili kurekebisha matatizo yote yarekebishwayo na vitamini hizi.Kuna kama vile magonjwa ya damu na mengineyo.

HUTIBU PUMU.
Tunda hili lina maji kiasi chacke ambayo kazi kubwa ni kuongeza unyevunyevu ndani ya mapafu na kupunguza uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa unaohusiana na njia hiyo ya hewa.Dawa nyingi za mitishamba ambazo hutumika kutibu pumu huchanganywa na unga wa zabibu zilizo sagwa na kukaushwa vizuri.

HUONDOA SUMU.
Viondoa sumu (anti-oxidants) ambavyo hupatikana kwenye tunda hili vina kazi kubwa sana kuachilia mbali nguvu inayotolewa kwenye maziwa.Mgonjwa ambaye amekunywa sumu mara tu na hakuna uwezekano wa maziwa jirani,unaweza kumpa juisi ya zabibu kama ipo jirani na hii itamsaidia.

HEREKEBISHA TATIZO LA DAMU.
Zabibu huongeza kiwango cha nitric acid mwilini ambacho huzuia damu kuganda.pia inaaminika kwamba juisi ya tunda hili inaongeza damu kwa mtumiaji anayeitumia mara kwa mara na husaidia kupunguza tatizo la moyo linalosababishwa na damu kuwa chache mwilini

HULAINISHA CHOO.
ukweli ni kwamba zabibu lina kiasi cha kawaida cha kamba lishe ambacho hufanya kazi ya kurekebisha choo kikubwa.Watoto wengi wanaokosa maji mwilini kutokana na wazazi kushindwa kuwapa maji ya kutosha,wanaweza kuanzishiwa utumiaji wa juisi ya tunda hili.

HUPUNGUZA MAFUTA MWILINI.
 Zabibu halina mafuta,hii husaidia kurekebisha uwingi wa mafuta yaliyomo ndani ya mwili kwani yana kiwango kikubwa cha carlories ambazo hushawishi matumizi ya mafuta kwa kuzalisha nguvu mwilini pindi ambapo zimekwisha carlories hizo.
  Tunda hili ni tamu na huweza kuliwa kwa kupitiliza kutokana na ladha yake,kumbuka kwa kufanya hivyo huendani na kanuni za afya bali unajiongezea uchafu mwilini kwani kiasi kidogo kinachohitajika kitachukuliwa na kilichobakia kitatolewa nje kama makapi ."Kula kwa afya na sio ule kwa kuwa kipo" nakumbuka zamani mama alikua anapenda sana kutumia maneno hayo akimaanisha nile kwa kiasi.

  Hata mimi leo sina budi kukushauri kwa matokeo thabiti ya afya yako tumia kiasi kidogo mara kwa mara kama ulivyoelekezwa hapo juu na hakika matokeo yake utayapata ndani ya muda mfupi.
Kwa ushauri,maoni au maswali kuhusiana na matatizo ya kiafya usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini....Ahsante.

PHONE;  0673666791

Email; goldamplat@gmail.com 

Jumatano, 25 Januari 2017

KAROTI.


          Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala haya,nakukaribisha tena ili kufahamu umuhimu wa tunda lingine aina ya Karoti.Ni tunda la tofauti kidogo kati ya matunda mengine ambayo tumekwisha yaona hapo awali lakini leo ngoja tuangalie umuhimu wa utofauti wake na matunda mengine.
   Kwanza hili ni tunda pekee ambalo linaweza kupikwa na lisiharibu ladha yake,pia linaweza kuliwa likiwa kama matunda mengine yanavyoliwa bila kupikwa.Pia tunda hili ni moja wapo kati ya matunda machache ambayo yanaoatikana chini ya ardhi,tumezoea matunda mengi hupatikana juu ya miti au hata yakiwa yamelala ardhini lakini sio chini ya ardhi kwa kufanya kuyafukua/kuchimba.

  Kuna aina tatu za karoti ambazo hutofautiana kwa rangi zake,kuna karoti nyekundu,ya njano na ya pinki lakini zote ni karoti.Karoti za njano na nyekundu ndizo zenye virutubisho vingi ukilinganisha na hiyo ya pink na mara nyingi ndizo aina za karoti ambazo hulimwa sana nchini kwetu Tz.
    Karoti kama yalivyo matunda mengine lina faida kubwa sana nyingi,watu wengi tumekua tukisikia faida moja tuu ya kutibu macho na kuyafanya yawe maangavu.Ni kweli lakini siyo kazi hiyo tuu bali kuna kazi nyingi za aina mbalimbali,ungana nami tuzione hapo chini;

 HUTIBU MATATIZO YA CHOO.
  Karoti lina kiasi kikubwa cha kamba lishe ambazo ndizo muhimu katika kurekebisha tumbo na kukupatia choo kizuri.Kambalishe hizi husaidia katika ufyonzaji wa maji katika njia ya mwisho ya usagaji wa chakula hivyo kukuweka katika hali nzuri kama zitapatikana kwa kiasi kikubwa mwilini.

 HULAINISHA NGOZI.
  Kwa mtumiaji wa karoti mara kwa mara atakubaliana na mimi kwa kazi hii ambayo karoti inafanya,warembo wengi wanatumia mafuta na losheni za ngozi zilizotengenezwa na tunda hili kwaajili ya umakini wa ngozi zao.Hii inatokana na uwepo wa vitamini E iliyopo ndani ya karoti inayofanya kazi ya kurudisha na kutengeneza seli mpya za ngozi zilizo haribika/kufa.

 HUFANYA MACHO KUWA MAANGAVU.
  Karoti ina kirutubisho kiitwacho Beta-carotenene ambacho ndio chanzo muhimu cha vitamini A mwilini.Baada ya kubadilishwa na kuwa vitamini A mwilini,carotenene hupelekwa moja kwa moja katika utengenezaji wa seli ndani ya pupil na retina kwenye macho.Hii hufanya uwingi wa seli hizi na kusababisha kuondoa tatizo la kutokuona kwenye mwanga hafifu au mdogo.

 HUONDOA TATIZO LA CHUNUSI.
  Kama tulivyoona hapo juu vitamin E ndiyo hasa itumikayo kupambana na magonjwa ya ngozi,hivyo kwa uwepo wa vitamini hii hutatua tatizo la chunusi na vipele vitokanavyo na mafuta mengi usoni.

CHANZO CHA NISHATI MWILINI.
 Karoti haina mafuta bali ina karolies nyingi,hivyo kwa mtumiaji wa karati hupata virutubisho hivi kwa wingi na kumfanya awe na nguvu za kumwezesha kuhimili kazi mbalimbali.

 HUREKEBISHA TATIZO LA DAMU.
  Juisi ya karoti inasifika kurekebisha tatizo la upungufu wa damu mwilini,kwa matumizi ya kama dawa unashauriwa kutumia ndani ya muda wa si chini ya miezi mitatu.Kunywa glasi moja ya juisi kila siku kwa matatizo ya damu.

  Karoti ni muhimu sana kwa watoto wadogo kwani ina vitamini A nyingi ambazo zitamjengea mtoto kinga nzuri juu ya magonjwa mengine mengi tofauti na ya macho.Unashauriwa kumwanzishia mtoto wako mdogo utaratibu wa kunywa juisi ya karoti kama dawa kwa kumkinga na monjwa mengine mengi.
Tunda hili limekuwa na sifa nyingi kutokana na kazi yake kubwa moja ya kutibu macho.
   Kwa kuwa na viondoa sumu vingi ndani ya karoti,imekuwa na mchango mkubwa wa kutibu magonjwa ya kansa kama vile kansa ya mapafu,tumbo na tezi za uzazi za kiume.
Kwa faida nyingine nyingi tazama; http://www.a2ztube.co.
  Kwa lolote linakusumbua kuhusu afya yako usisite kuwasiliana nasi kwa ushauri na kukujibu maswali yako.Pia tunatoa huduma za kufundisha taratibu za milo mingine kwa ajili ya matatizo ya afya yatokanayo na mfumo wa maisha...Ahsante.

PHONE;  0673666791

Email: goldamplat@gmail.com

Jumapili, 22 Januari 2017

 TIKITI-MAJI.



     Leo tena katika makala nyingine tunakutana kuzungumzia tunda aina ya Tikiti-maji,kabla ya kuanza mada yetu hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea na kutuweka salama mpaka muda huu.Ni matumaini yangu ni wazima wa afya na mmejaaliwa kuiona siku nyingine hivyo sifa na utukufu arudishiwe Mungu muweza yote.

  Kama wengi jinsi tunavyolifahamu tunda hili kuwa na uwingi wa 92% ya maji pekee ndivyo kazi yake kubwa yakuhakikisha maji mwilini mwa mtumiaji hayapungui.Tikiti-maji lina aina mbalimbalio za madini ambayo hufanya kazi nyingi mwilini mwetu na kusaidia kuboresha afya ya mlaji.
Tuangalie baadhi ya kazi muhimu za tunda hili;

HUONGEZA NGUVU ZA KIUME.
 Kila kipatikanacho ndani ya tunda hili kina kazi kubwa ukianzia majani,maganda pamoja na mbegu.Wanaume wengi wamekua wakikumbwa na tatizo la hili na kumekuwa na matangazo mbalimbali kuhusiana na dawa za kusaidia tatizo hili.Ndugu msomaji ni bora kutumia dawa za matunda/lishe ili kutibu au kupunguza au kuzuia tatizo lako na sio kila dawa kuiona inafaa.Mbegu za tunda hili zikiliwa pamoja na nyama ya tunda hili husaidia katika kurekebisha upungufu wa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa kuliko inavyotegemewa.Watu wengi wamejaribu kufanya hivyo na matokeo wamerudisha sifa na shukrani kwa somo hilo,tuwasiliane kwa maelezo zaidi.

HUONDOA SUMU MWILINI.
  Lycopene ipatikanayo ndani ya tunda hili husaidia kuzuia sumu mbalimbali mwilini zisiudhuru.Pia sumu zipatikanazo kwenye baadhi ya nyama (protini) hurekebishwa kwa kirutubisho hiki.Pia baadhi ya protini ngumu tunazokula kila siku husagwa nakufanywa nyepesi kuchukuliwa ndani ya mwili na kufanya kazi husika kuliko kutolewa nje kama uchafu/kinyesi.

HUSAIDIA MATATIZO YA CHOO NA UPUNGUFU WA MAJI.
 Kuwepo kwa maji kwa asilimia nyingi pamoja na kamba lishe,kunasaidia kurekebisha matatizo ya choo na kibofu cha mkojo.Kwa wenye magonjwa haya,kwa kutumia tunda la Tikiti-maji wataweza kuyatibu na kuyazuia na kwa wale ambao hawana wanashauriwa kutumia tund hili ili kujihakikishia ulinzi wa afya zao na wasisubiri mpaka wakutane nayo.

HUPUNGUZA SHINIKIZO LA DAMU KWA KIWANGO KIKUBWA.
 Utafiti uliofanywa na watu wamarekani ulibaini kuwa watu wengi walio na tatizo la shinikizo la damu (PRESURE) na wakatumia tunda hili katika milo yao waliweza kupunguza kasi ya tatizo hilo.
Hii inatokana na uwepo wa sukari asilia ambayo ni muhimu kurekebisha kiwango cha sukari mwilini na kukuleta kiwango sawa cha sukari inayohitajika.

MAGONJWA YA MENO NA MIFUPA. 
  Tikiti-maji lina madini kama vitamini C ambayo husaidia kuzuia magonjwa ya fizi pamoja na meno (KISEYEYE),hivyo ulaji wa tunda hili hasa kwa watoto utapunguza kasi ya athari za ugonjwa huu.
Watoto wengi pia hulipenda kutokana na sukari yake iliyomo ndani ya tunda hili hivyo haitakua vigumu mtoto kulila kwani kuna baadhi ya matunda ambayo sio rafiki kwa watoto na asilimia kubwa hayapendwi kutokana na uchachu,uchungu au kiwango kidogo cha sukari kinachopatikana.

HUIMARISHA UBONGO.
 Uwepo wa vitamini Bcomplex (B6) kwenye tunda hili husaidia kuimarisha kazi ya ubongo na kuufanya kuwa mchangamfu kwa muda mrefu.Baadhi ya matatizo yanayoyaukumba ubongo huweza kuzuiwa na kurekebishwa na vitamini hiyo.Unashauriwa kama wewe ni mwanafunzi utumie tunda hili kwa manufaa ya kuufanya ubongo wako kuwa active.Vilevile hata kwa wazee na walevi wanaokutana na matatizo ya kusahau watakuwa vizuri endapo watatumia tunda hili.Si kuimarisha tuu bali tunda hili hutumika kama lishe ya ubongo.


   Siyo ivyo tuu,licha ya kuchangia kwa kiasi kikubwa urekebishaji wa tatizo hilo tunda hili lina uwezo mkubwa sana wa kusaidia moyo kuweza kufanya kazi kwa kiwango sahihi na sio kuzidiwa na kazi.Hii husababisha kuupa moyo muda wa kutosha wa kupumzika kwa kufanya kazi kidogo.
  Unaweza aukatumia tunda hili kama juisi na pia ukala kama unavyokula matunda mengine ila vyote hufikisha virutubisho mwilini,lakini pia kwa matatizo mengine ambayo tumeyaona hapo juu unashauriwa kutengeneza juisi ya tunda hili bila kuondoa kitu chochote kile nikimaanisha kuanzia maganda mpaka mbegu zake.
      Anza mazoea sasa yakutumia matunda kama lishe mbadala na kinga dhidi ya magonjwa na usisubiri mpaka ukutane na magonjwa ndipo ukumbuke kuna lishe ya matunda,fanya hivyo kwa manufaa ya afya yako binafsi na sio kwa kulazimishwa wala kuiga ulaji wa mtu mwingne.
Ifahamike wazi kwamba ulaji wa matunda kiafya haukusababishii wewe usimwone daktari,bali kuna matatizo mengine ambayo ni lazima ukafanyiwe uchunguzi na ukatibiwe kwa mtaalamu wa afya kwani yanaweza kuwa ni zaidi ya ufikiriavyo.
 Kwa maoni,ushauri na mengineyo usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini. Ahsante

PHONE:  0673666791

Email: goldamplat@gmail.com

Jumatano, 18 Januari 2017

FENESI.

   Kama ilivyo ada ni wasaha mwingine ambao tunamshukuru mungu kwa kutupa uzima na kukutana tena katika makala yetu ya kila siku.Tunapaswa kumshukuru mungu kwani bila yeye hakuna ambalo tunalifanya na kuwa sahihi
Leo nitakupeleka moja kwa moja kuona umuhimu wa tunda aina ya fenesi kiafya ya ndani na nje ya mwili.
 
    Tunda la fenesi ni moja kati ya matunda yenye sukari kwa kiasi chake,ulaji wa 100g za fenesi hukupa karolizi 90 kutokana sukari aina ya fructose na sucrose zilizomo ndani ya tunda hili.Kutokana na ukweli kwamba matunda mengi huwa na virutubisho vingi vinavyofanana hasa vitamini C,utaona kazi nyingi za baadhi ya matunda pia hufanana.Tuangalie faida za tunda hili kiafya kama ilivyo kawaida yetu:

MAGONJWA YA MOYO.
Sababu mojawapo ya magonjwa ya moyo ni pamoja na sukari kuwepo kwa wingi ndani ya mzunguko wa damu hii husababisha kuongezeka kwa kasi ya usafirishaji wa damu na mapigo ya moyo (blood pressure).Hii hupunguzwa kutokana na tunda la fenesi kuwa na kiwango cha sukari ambayo husaidia kurekebisha sukari mwilini.Hata hivyo mafuta yapatikanayo ndani ya fenesi hayana lehemu,hivyo ni mafuta sahii kutumika na yana uwezo mkubwa wa kukabiliana na tatizo la pressure hasa ya kupanda.
 
HUTIBU TATIZO LA DAMU.
Uwepo wa potasium na baadhi ya madini kama folic acid ndani ya tunda hili husaidia kwa kiasi kikubwa kusulihisha suala la damu.Kwa kuwa na anti oxidant Fenesi husaidia kuondoa sumu mwilini na kukupunguzia kasi ya magonjwa ya kansa na kulipunguzia ini kazi nzito ya kupambana na sumu mwilini.

MIFUPA NA MENO.
Mifupa huwa dhaifu kutokana na umri,vyakula tunavyokula pamoja na maradhi lakini vyote hivyo huweza kuepukika kama utaamua kuanza leo afya lishe na tunda hili.Fenesi lina madini mengi ya magnesium na kalisium ambayo husaidia kwa kiasi fulani katika kuimarisha mifupa.Hata magonjwa ya meno hutibiwa kwa fenesi kwani lina kiwango kikubwa cha vitamini Cambayo hufanya kazi nzuri katika kuimarisha uimara wa meno.
 
HULINDA NGOZI.
Dawa sahihi ya ngozi zilizojikunja (kama za wazee) ni Fenesi,hii ni kutokana na kiasi kikubwa cha mafuta ambacho tunda hili kinacho ambacho husaidia katika kulainisha ngozi na kuipa muonekano mwaroro.Sio hadithi za dhahania bali ni ukweli kwamba mafuta ya ngozi yatokanayo na fenesi ndio yaliyothibitishwa kuwa mafuta bora kwa afya ya ngozi ya binadamu.Fenesi huipa ngozi mwonekano kama wa ngozi ya mtoto mdogo,hivyo kwa akina dada si vyema sana kuhangaika na vipodozi vyenye madhara na gharama kubwa bali ubadilishe mazoea na kuanza kutumia fenesi kwa uzuri wa ngozi yako.
 
UNG"AAVU WA MBONI ZA MACHO.
Kutokana na uwepo wa vitamini A ambayo kazi yake kubwa ni kuyafanya macho yawe na uwezo mzuri wa kuona,pia hupatikana ndani ya tunda hili nakufanya kuwa na kazi muhimu ambayo inahitajika kila siku kwani tatizo la macho kwa kiasi kikubwa huathiri mwenendo mzima wa maisha yetu ya kila siku.
      Ulaji wowote uliopitiliza ni hatari kwa afya yako hata kama kitu hicho kitakua na faida mara mia,unatakiwa kula kistaarabu na kwa kiasi na sio kwamba umejua kuna faida za kutumia chakula hicho ukatumia zaidi.Mchanganyo wa fenesi na vyakula vingine huleta sumu ndani ya mwili wako,kaa na taadhari
 ONYO: USIJARIBU KULA FENESI NA KUNYWA SODA YA COCOA-COLA KWA MFUATANO.
 Kufanya hivyo unahatarisha maisha yako kwa muda mchache sana,kwani mchanganyiko huo husababisha utengenezwaji wa sumu ifananayo na nyoka aina ya cobra.
Utafitii uliofanyika china umedhihirisha jambo hilo:

 Kwa mapendekezo,maoni,maswali na ushauri wowote  juu ya tatizo lolote kuhusiana na AFYA usisite kuwasiliana nasi muda wowote.
PHONE:        0673666791


Jumanne, 17 Januari 2017

NANASI.

 

     Leo tena katika makala nyingine tunakutana kuzungumzia tunda aina ya nanasi,kabla ya kuanza mada yetu hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea na kutuweka salama mpaka muda huu.Ni matumaini yangu ni wazima wa afya na mmejaaliwa kuiona siku nyingine hivyo sifa na utukufu arudishiwe Mungu muweza yote.
   Nanasi kama linavyojulikana kwa jina lingine la Pineapple ni tunda linalopendwa na watoto wengi kwani lina sukari nyingi ukilinganisha na matunda mengine.Licha ya watoto pia hata watu wazima wanapenda sana juisi ya nanasi kutokana na utamu wa ladha iliyokua nayo.Tunda hili ni miongoni mwa matunda yanayoongoza kutibu magonjwa ya koo na yamekuwa yakitumika na wengi kutokana na kazi hii.Baada ya kumenywa vizuri na kuwa tayari kwa kuliwa,nanasi halitakiwi kuhifadhiwa ndani ya friji kwani hupoteza ubora wa virutubisho vyake bali kwa kuliweka katika chombo chenye mfuniko na kulihifadhi vizuri hulipa thamani yake sahihi hata kwa muda wa zaidi ya siku nne.
   Kama yalivyo matunda mengine,nanasi linaweza kuliwa kama jinsi lilivyo au likatengenezewa juisi,njia zote ni sahihi katika kupata virutubisho sahihi vya tunda hili.Tuangalie umuhimu wake katika kutibu na kuzuia baadhi ya magonjwa;

MAGONJWA YA KOO.
 Tunda hili limeonekana kuweza kupambana na ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo

MAGONJWA YA TUMBO.
 Udhaifu wa tumbo kushindwa kusaga chakula hasa protini hurekebishwa na tunda la nanasi.Hii ni kutokana na uwepo wa kimeng"enya cha aina ya Bromelain ambacho hufanya kazi kubwa ya kusaidia kusaga vyakula vilivyo na ugumu katika usagaji wake.Hii hupelekea tatizo hilo kutatuliwa na tunda hili hivyo kulifanya kuaminika na watu wengi katika kutatua tatizo hilo.

KULAINISHA CHOO.
 Kamba lishe zilizomo ndani ya papai husaidia tatizo la choo na kutoa choo laini na sio kigumu.Kwakua nanasi lina majimaji kwa kiasi kingi huweza kuzuia tatizo la uhaba wa maji katika mfumo wa chakula mwilini mwa binadamu.Kwa ushauri wa tatizo hili tumia nanasi na uone mafanikio sasa

HUONGEZA DAMU.
 Nanasi lina kiasi fulani cha madini chuma ambayo husaidia katika kuongeza damu kwani huusika na utengenezaji wa damu mwilini mwa binadamu.wagonjwa wengi waliopungukiwa na damu hushauriwa kutumia tunda hili kaam njia mbadala ya kuongeza damu mwilini mwao.
 

BARIDI YABISI (ATHRITIS).
 Baadhi ya magonjwa ya baridi yabisi yaani magonjwa ya jointi hutatuiliwa kwa ulaji wa nanasi kutokana na uwingi wa vitamini zilizomo kwenye tunda hili kama vile vitamini A,B, na C.Wazee wengi huwa na tatizo hili hivyo hushauriwa kutumia nanasi kwa kutatua tatizo hili.

     Uwepo wa vitamini hizo husaidia kukabiliana na magonjwa mengine kama ya fizi,meno na magonjwa mengine ya mifupa na sio magonjwa machache niliyoyaelezea hapo juu tuu bali na mengine ambayo tutazidi kuelezana kadri tunavyokua pamoja.

     Kuna dhana inayosikika kwamba nanasi si tunda bora kwa akina mama wajawazito kwani huwaletea matatizo,jambo hilo sio la kweli na ni kama hadithi zilizo simuliwa zamani za mababu zetu za kukataza mama mjamzito kutumia baadhi ya vyakula fulani.
Tumia nanasi ukiwa na lengo la kuboresha na kuimarisha afya yako na sio kwa mazoea ya kula ilimradi umekula.
   Fuata kanuni na taratibu sahihi za afya kwa matokeo sahihi ya afya bora na sio kufanya kwa mazoea,mfundishe mwanao,rafiki na hata jirani yako juu ya umuhimu wa tunda hili naye anufaike.
Kwa mtazamo na maoni yoyote juu ya jambo lolote lihusianalo na afya yako usisite kuwasiliana nasi kwa namba hapo chini,Ahsante.

  PHONE; 0673666791
  Email; goldamplat@mail.com

Jumatatu, 16 Januari 2017

MACHUNGWA


        Habari ndugu msomaji ni matumaini yangu u mzima wa afya na Mungu amekujal;ia afya iliyo imara,kama ni mgonjwa pia unatakiwa kumshukuru mungu na kuangalia wapi ulikosea kufuata kanuni za afya na ujirekebishe ili kurudia katika hali yako ya uzima.
Leo tutaangalia umuhimu wa tunda aina ya Chungwa kwani wengi wamekua wakiniuliza baadhi ya maswali kuhusiana na tunda hili.
    Kwanza kabisa tunda hili halitakiwi kuliwa na mtu mwenye vidonda vya tumbo kama hajala kitu chochote kwani ni aina ya tunda lenye asidi ambayo inaweza ikamletea matatizo katika vidonda vyake.Pia mbegu za tunda hili licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini,vitamini na madini mengine,zinz kiwango kikubwa cha sumu aina ya Cynide (sayanid) ambayo kama itapatikana kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu ni sumu ambayo inaweza kuua kwa haraka.
 Faida za virutubisho ambavyo vipo ndani ya chungwa hupatikana katika sehemu kuu mbili nazo ni Maji ya chungwa (mchuzi wa chungwa) na kwenye nyama ya chungwa.Unashauriwa kula chungwa lote na sio kukamua maji yake na kisha kulitupa kwani utakosa kambalishe zipatikanazo kwenye nyama ya chungwa.Watoto wadogo hufanya hivyo mara nyingi,sio inamaanisha wanakosa virutubisho vyote hapana! bali wanapata vichache vile vilivyomo ndani ya mchuzi pekee.
 Hivyo na kwa wewe ambae ulikua huafahamu jambo hilo sasa umelifahamu na nina imani utabadilika na kulifanyia kazi kwa manufaa ya afya yako mwenyewe.
   Hata hivyo licha ya yote hayo bado tunaona tunda hili lina faida mbalimbali mwilini kama vile;

UKOSEFU WA CHOO.
 Uwepo wa kambalishe ndani ya tunda hili husaidia katika usagaji wa chakula na kuondoa kabisa tatizo la choo.Pia kolesto zilizopo mwilini hupungua kwani umuhimu wa kambalishe hizi huonekana katika usagaji wa chakula na kusababisha mafuta yote yaliyozidi mwilini kutumika kwa kuyeyushwa na hivyo kufanya tatizo hili lisiwepo kabisa.
 
MAGONJWA YA MOYO.
 Flavonoidi pamoja na vitamini C inatopatikana ndani ya tunda hili husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kama vile mafuta kujaa ndani ya mishipa ya moyo kama tulivyoona hapo juu.
 
MAGONJWA YA MENO NA FIZI.
 Uwepo wa vitamini C ambayo husaidia katika kupambana na magonjwa ya udhaifu wa meno na fizi,utakusaidia katika kuimarisha afya ya meno na fizi zako kwa ujumla.

MAGONJWA YA MAPAFU.
 Chungwa lina kiasi kikubwa cha vitamini B6 na madini ya chuma ambayo husaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu ambazo huusika na usafirishaji wa hewa safi mwilini.Hii huondoa matatizo ya mapafu na mzunguko wa hewa safi mwilini moja kwa moja.

SHINIKIZO LA DAMU.
 Machungwa ni muhimu kwa wagonjwa wenye shinikizo kubwa la damu (presha) kwani kwa kuondoa mafuta yaliyorundikana kwanye mishipa ya damu pamoja na kuwa na virutubisho vya magnesium huondoa kabisa tatizo hili na kufanya mwenye tatizo kama hilo kupona na kujisikia vyema.
   Si mpaka uwe mgonjwa ndio uanze kutumia machungwa na matunda mengine bali kinga ni bora kuliko tiba.Ni bora kujiwekea mazoea ya kula matunda kwa wingi ili kupata virutubisho vinavyohitajika vikawe kama akiba ya baadae na kinga kwa magonjwa nyemelezi.

MAGONJWA YA FIGO.
 Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kurekebisha Ph ambayo itakufanya uwe na hali iliyo timilifu ndani ya mwili wako hii hulipumzisha ini pamoja na figo katika kufanya kazi nzito ya kurekebisha na kupambana na hali inayobadilika mara kwa mara.
 
KUONDOA CHOLESTEROL.
 Uwepo wa kirutubisho cha lemonin ndani ya machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa sana kuondoa mafuta ambayo hayahitajiki ndani ya miili yetu.Hasahasa kwa watu wanene kupita kiasi (obese) wanaweza wakapunguza unene huo kwa kufuata utaratibu wa matumizi bora na sahihi ya matunda kama machungwa na mengineyo.

   Ulaji wa chungwa pia umetofautiana kama tulivyoona hapo juu,hivyo unaweza ukaamua wewe utumie tunda hili kama juisi au kama tunda la kawaida kulila.Na pia ulaji wake tumeuangalia hapo juu hivyo nakushauri uache kula kwa mazoea, na uanze kula kwa faida ya afya na sio ladha pekee.
Kwa ushauri na tatizo lolote linalohusiana na afya yako usisite kuwasiliana nasi muda wowote na pia kama una maoni,ushauri na vyovyote uonavyo wewe wasilisha kwa mawasiliano yetu hapo chini.Mungu akubariki.

    PHONE: 0673666791

    Email: goldamplat@mail.com

                www.amplatblogspot.com

Ijumaa, 13 Januari 2017

EMBE
Uhali gani ndugu msomaji wa makala haya,ni matumaini yangu u mzima wa afya na mugu amekujalia kuamka salama hivyo tunapaswa kumshukuru kwa neema hii.Twende moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo inayohusiana na tunda aina ya embe.


Katika matunda yenye sukari ni pamoja na tunda hili,ukiachilia mbali ndizi,nanasi na mapera.wengi wetu hupenda kulitumia tunda hili kama kutengenezea juisi,kulila likiwa limeiva au bichi na hata bidhaa za vindani kama vile achali na mango pickle.Wote huu ni ulaji ambao unaongeza virutubisho mwilini vilivyo katika embe.Faida nyingi huonekana katika ulaji wa embe na sio tuu nyama yake bali hata miziz,majani pamoja na maua yake pia,tuone baadhi.
MAGONJWA YA MACHO.
Embe lina vitamini A kwa kiwango kikubwa baada ya karoti ukilinganisha na matunda mengine,uwezo huu husaidia kudhibiti magonjwa ya ukavu macho na udhaifu mwingine wa macho.tumia embe kwa lengo la kutibu macho yako na sio kwa mazoea ya kula kwa kujifurahisha.

UDHAIFU WA TAYA NA MENO.
Uwepo wa vitamini C katika tunda hili,unahakikisha kazi ya uimarishaji wa meno na taya/fizi za meno.Kwani vitamini C huzuia ugonjwa wa udhaifu wa meno (scurvy).kula embe kawaida unaweza kulila likiwa lenyewe au ukatengeneza juisi ya tunda hili.

MALARIA SUGU.
Majani machanga ya mti wa muembe hutumika kama kinga na tiba ya malaria sugu kwa asilimia kubwa.Unaweza kuyatumia kwa kuyatafuna baada ya kuyaosha vizuri au pia unaweza kuyachemsha na kuyaacha yapoe kwa muda ndipo uyatumie maji na majani yenyewe.
NB: Katika kutibu ugonjwa huu hakikisha unakula majani haya machanga kwani yana nguvu kubwa ya kupambana na wadudu wa malaria sugu.

PUMU.
Majani ya muembe yakikaushwa vizuri katika kivuli (ili kuzuia alkadosisi kupotea) na kusagwa pia hutumika katika kutibu tatizo la pumu.Hii imewasaidia wengi katika kufanya ivyo na wameondokana na tatizo hilo.Saga majani hayo na uchanganye na maji kisha uyatumie kwa kunywa utapata matokeo.

MATATIZO YA UZAZI.
Tunda hili lina kokwa ambalo ndio dawa kubwa ya tatizo la kuziba mirija ya uzazi na tatizo hili haliwapati akina mama tuu bali hata kwa akina baba nao hukumbwa nalo.Chukua kokwa likaushe vizuri na ulisage ili kupata unga wake,halafu tumia unga huo kuchanganya na maji kisha kunywa hayo maji angalau glasi moja kabla ya mlo wako wowote ule.

Matatizo mengine kama ufinyu wa utoaji maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha huondolewa kwa kutumia maua ya maembe,pia hata harufu mbaya ya mdomo huondolewa kwa matumizi ya majani ya maembe.
Utumiaji wa tunda hili kama dawa utaona mabadiliko yake ndani ya muda mfupi kama ukizingatia utaratibu wa lishe kiafya na sio kwa mzoea.
Nikushukuru kwa muda wako wa kusoma na nikuombe uanze kufanyia kazi kama kweli unataka mabadiliko kiafya na si uchukulie kawaida kama ulivyozoea.
Kwa ushauri,maoni na matatizo yoyote yahusuyo afya yako,usisite kuwasiliana nasi kwa;

Phone; 0673666791
Email; goldamplat@gmail.com amplat afya kwanza

Jumatano, 11 Januari 2017

 PAPAI


Habari za muda huu ndugu msomaji,naamini u mzima wa afya na furaha hivyo huna budi kumshukuru Mungu.Kwa wale walio na matatizo ya kiafya na kiakili nao hawana budi kumshukuru mungu kwani pumzi waliyopewa kwa siku ya leo inatosha kabisa kusema asante kwa Mungu wako.
   Leo tutaangalia umuhimu wa tunda la aina nyingine,ambalo ni papai.tunda hili pia sio geni na linafahamika na idadi kubwa ya watu nchini kwetu.Lichz ya kuwa watu wengine hula tunda hili kutokana na utamu wa sukari iliyomo ndani mwake,lakini ukweli kwamba tunda hili lina virutubisho vingi ambavyo vitakufafanya uwe na afya bora na uondokane na magonjwa mbalimbali,tuanze kuangalia tatizo moja baada ya lingine.

USAGAJI WA CHAKULA MWILINI.
 Watu wengi wanaopata choo kigumu ni wavivu wa kunywa maji,labda hawaoni umuhimu wake au wana mazoea ya kunywa maji pale wasikiapo kiu tuu.Utaratibu huu sio mzuri ingawa umezoeleka na watu wengi hivyio ni lazima tupingane nao.Kutokana na ulaini wa papai na kimeng"enya cha PAPAIN kilichopo ndani ya tunda hili,husaidia kulainisha chakula tumboni na kukifanya kiweze kusagika kwa urahisi zaidi.Ili uondokane na tatizo la usagaji wa chakula na magonjwa mengine yahusikayo na hayo,huna budi kutumia papai na kujizoesha kunywa maji mara nyingi uwezavyo kwa siku.Si tuu kwa ajili ya tatizo hili bali na matatizo mengine pia.


MAGONJWA YA UKOSEFU WA VITAMINI.
 Katika matunda yenye utajiri wa vitamini,papai ni mojawapo katika orodha kwani lina vitamini A,B,C,D na E.vitamini zote hizo hutumika kurekebisha magonjwa kama ukavu macho,kiseyeye na matege (kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5).Vilevile magonjwa mengine ambayo sijayataja hapo juu yatokanayo na ukosefu wa vitamini hizo huzuiliiwa kwa kula papai kwani litasababisha uwepo wa vitamini hizo na kuzuia magonjwa hayo kutokea.

UPONYAJI WA VIDONDA.
 Ute ute/Maziwa ya papai hutumika kutibu vidonda vya aina zote,kuanzia vidonda vya ndani ya mwili hata vile vya nje ya mwili wa binadamu.Vidonda kama vya tumbo huweza kutibiwa kwa maziwa hayo yatokanayo na papai vile vile hata vidonda vya nje kama kuungua na kuumia sehemu fulani ya mwili hutibiwa kwa kupaka mafuta hayo sehemu iliyoathirika/yenye jeraha.
 

MAGONJWA YA INI NA FIGO.
 Ini ndio ogani pekee ambayo hupambana na sumu mwilini mwa binadamu,ukiachilia mbali figo ambayo kwa kiasi fulani huondoa sumu.Mbegu za papai hulipa ini nguvu za kuendelea kupambana na sumu ziingiazo mwilini mwetu na kukupunguzia kiwango kikubwa cha sumu ambazo zitaathiri afya yako.Pia majani ya mpapapi yakichemshwa kwa dakika 15 na kuutumiwa kwa kunywa angalau lita 1.5 kwa siku,husafisha kabisa figo na kuondoa matatizo yatokanayo na mfumo wa utoaji taka mwili (mfumo wa mkojo)

MAGONJWA YA MAPAFU.
  Kwa watumiaji wa sigara na wale wote wanaokumbana na adha za moshi kila kukicha,utumiaji wa papai utakupunguzia madhara ya moshi kwa asilimia kubwa (zaidi ya 80%).Kutokana na vitamini A iliyopo kwa wingi ndani ya tunda hili madhara yatokanayo na moshi huzuilika,kwani tunajua wazi kwamba moshi huathiri mfumo wa upumuaji wetu kwani ni hewa mbaya ambayo inaingia mwilini (kwenye mapafu) na kuingilia mfumo mzima wa upumuaji.
Wagonjwa wa macho pia nawashauri kutumia papai kama dawa na sio kama mlo wa mazoea tena,kwani kwa kufanya hivyo utajihakikishia usalama na uhai wa afya yako.
 Kwa ushauri na matatizo yanayohusu afya yako,wasiliana nasi muda wowote upate ushauri.Pia tunakaribisha maoni,mapendekezo na mitazamo mbalimbali.

Contact: 0673666791
Email: goldamplat@mail.com

Jumapili, 8 Januari 2017


       TANGO

Image result for faida za tango kiafyaImage result for faida za tango kiafya

Habari za tangu tulipokuwa pamoja muda uliopita,ni matumaini yangu ni wazima wa afya na hatuna budi kumshukuru mwanyezi mungu.Kwa wale walio wagonjwa na hawajiwezi mungu awasaidie na niwape pole pia.
Tuanze na mada yetu muhimu ya kutambua umuhimu wa virutubisho vipatikanavyo ndani ya matunda.Tuanze na umuhimu wa Tango,kama tunavyolifahamu tunda hili ni muhimu kwa afya kwani lina kazi nyingi sana katika miili yetu.maganda yake na mbegu zake ndio huwa na umuhimu mkubwa kama tutakavyoona.




Tunapoongelea umuhimu wa tango tunaona uwezo wake mkubwa katika kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali kama vile;

MAGONJWA YA NGOZI.
Tango hujulikana kwa kuwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha ngozi,tangu zamani tunda hili lilitumika katika kutibu magonjwa ya ngozi.Weusi upatikanao kuzunguka maeneo ya macho,huweza kuondolewa kwa kutumia vipande kadhaa vya tango.Chukua vipande viwili vya tango na usugulie kuzunguka eneo lenye weusi,kwa kufanya hivyo utaweza kutibu eneo hilo.

HARUFU MBAYA MDOMONI.
Kama kinywa chako kinatoa harufu mbaya na unashindwa kuzuia,unaruhusiwa kutumia kipande kimoja hadi viwili kwa kutafuna.Kwa kufanya hivyo utazuia harufu mbaya mdomoni.

KUONGEZA UTE KWENE JOINTI.
Ifahamike kwamba maji yapatikanayo kwenye tango husaidia pia katika kuongeza uteute katika joint za mwilini.Hii huzuia mifupa kusagana na hivyo matatizo ya mifupa kushughulikiwa ipasavyo.kula tango kwa lengo la kutibu matatizo na sio kwa mazoea.

  Faida nyingine za tango ni kama vile,kusafisha kiatu cha rangi nyeusi na kufanya king"ae zaidi.Tango lina vitamini B1,B2,B3,B4,B6 na B12 pia lina kashiumu na potashium kwa wingi.