Alhamisi, 26 Januari 2017

ZABIBU.




     Ni matumaini yangu u mzima wa afya na unaendelea na majukumu yako ya kila siku katika kujenga nchi yenye nguvu.Nchi imara haiwezi kuja kama wajenzi wake wana afya dhaifu itakua ni dhahania hivyo hakikisha unafuata kanuni za mlo wa afya na kinga mwilini mwako ili kupata afya iliyo thabiti.
  Leo mezani kwangu nimekuandalia tunda lingine ambalo ni moja kati ya tunda la karne na karne lenye sifa na uwezo mkubwa,nalo si lingine bali ni Zabibu.

  Katika matunda yaliyojizolea umaarufu mkubwa kuanzia karne ya sita ni tunda hili.ni la zamani sana na lilitumika kutengenezea pombe (mvinyo) tangu enzi za watu wa kale.Kusema ukweli tunda hili ni tamu na linapendwa na kila mtu hasa hasa na watoto.
  Kuna aina tatu ya zabibu nayo ni zabibu za kijani,nyekundu na kama nyeusi (dark-red),aina zote hizi huliwa kwa njia mbalimbali kama vile kwa kutengenezewa juisi,zabibu zilizo kaushwa kama raisin na kama tunda la kawaida  kama matunda mengine.Tuangalie faida kuu za tunda hili;

 VITAMINI B COMPLEX.
  Karibu aina zote za vitamini B unazozifahamu zipo humu kwenye zabibu,hii inalipa sifa tunda hili kurekebisha matatizo yote yarekebishwayo na vitamini hizi.Kuna kama vile magonjwa ya damu na mengineyo.

HUTIBU PUMU.
Tunda hili lina maji kiasi chacke ambayo kazi kubwa ni kuongeza unyevunyevu ndani ya mapafu na kupunguza uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa unaohusiana na njia hiyo ya hewa.Dawa nyingi za mitishamba ambazo hutumika kutibu pumu huchanganywa na unga wa zabibu zilizo sagwa na kukaushwa vizuri.

HUONDOA SUMU.
Viondoa sumu (anti-oxidants) ambavyo hupatikana kwenye tunda hili vina kazi kubwa sana kuachilia mbali nguvu inayotolewa kwenye maziwa.Mgonjwa ambaye amekunywa sumu mara tu na hakuna uwezekano wa maziwa jirani,unaweza kumpa juisi ya zabibu kama ipo jirani na hii itamsaidia.

HEREKEBISHA TATIZO LA DAMU.
Zabibu huongeza kiwango cha nitric acid mwilini ambacho huzuia damu kuganda.pia inaaminika kwamba juisi ya tunda hili inaongeza damu kwa mtumiaji anayeitumia mara kwa mara na husaidia kupunguza tatizo la moyo linalosababishwa na damu kuwa chache mwilini

HULAINISHA CHOO.
ukweli ni kwamba zabibu lina kiasi cha kawaida cha kamba lishe ambacho hufanya kazi ya kurekebisha choo kikubwa.Watoto wengi wanaokosa maji mwilini kutokana na wazazi kushindwa kuwapa maji ya kutosha,wanaweza kuanzishiwa utumiaji wa juisi ya tunda hili.

HUPUNGUZA MAFUTA MWILINI.
 Zabibu halina mafuta,hii husaidia kurekebisha uwingi wa mafuta yaliyomo ndani ya mwili kwani yana kiwango kikubwa cha carlories ambazo hushawishi matumizi ya mafuta kwa kuzalisha nguvu mwilini pindi ambapo zimekwisha carlories hizo.
  Tunda hili ni tamu na huweza kuliwa kwa kupitiliza kutokana na ladha yake,kumbuka kwa kufanya hivyo huendani na kanuni za afya bali unajiongezea uchafu mwilini kwani kiasi kidogo kinachohitajika kitachukuliwa na kilichobakia kitatolewa nje kama makapi ."Kula kwa afya na sio ule kwa kuwa kipo" nakumbuka zamani mama alikua anapenda sana kutumia maneno hayo akimaanisha nile kwa kiasi.

  Hata mimi leo sina budi kukushauri kwa matokeo thabiti ya afya yako tumia kiasi kidogo mara kwa mara kama ulivyoelekezwa hapo juu na hakika matokeo yake utayapata ndani ya muda mfupi.
Kwa ushauri,maoni au maswali kuhusiana na matatizo ya kiafya usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini....Ahsante.

PHONE;  0673666791

Email; goldamplat@gmail.com 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni