Jumanne, 7 Februari 2017

PERA



     Ni wakati mwingine ndugu mpenzi mfuatiliaji wa makala haya tunakutana tena kuelekezana kuhusu faida za lishe ya matunda mbalimbali.Leo tutaangalia umuhimu wa tunda la aina ya pera kwani wengi wamekua wakiniuliza kuhusiana na faida za tunda hili hata kabla sijachukua maamuzi ya kuliandika na kulitolea ufafanuzi
 Kwanza tuanze kumshukuru mungu kwa yote aliyotutendea na kutufikisha hapa tulipo kwa siku ya leo,kama ni mgonjwa unapaswa kumshukuru mungu pia na kutafuta njia gani ufanye ili uondokane na ugonjwa huo.Twende pamoja katika kuangalia faioda mbali mbali za tunda hili;

 Kama tunavyolifahamu tunda la pera ni tunda ambalo watu wengi hawapendi kulila kawaida kwani lina mbbegu ambazo ni ngumu sana ambazo hata watoto wadogo hawawezi kuhimili kuzitafuna.Kuna pera la kijani,njano na jekundu yote haya ni sahihi kuliwa lakini yanaonyesha hatua za ukomavu wake,lakini kwa pera la kijani mara nyingi huwa linakua bado bichi hivyo ukila pera hilo utasumbuliwa na tumbo kwani virutubisha vyake huwa bado havijakamilika.
     Licha ya kuwa na sifa hiyo hakumaanishi eti usle kabisa tunda hili hapana,unaweza ukalisaga na kutengeneza juisi ambayo itakufanya upate virutubisho vile vile ambavyo ungevipata kwa kulila likiwa lenyewe.Pera kama yaaalivyo matunda meeengine lina faida mbali mbali kama vile;

VITAMINI C
 Tumeona tangia mwanzo faida za vitamini C kwenye mwili wa binadamu na kama utakumbuka vizuri ni karibia kila aina ya tunda lina kirutubisho hiki hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kwamba matunda ni chanzo kikubwa cha vitamini C.Kazi kubwa ya kirutubisho hiki ni pamoja na kuzuia magonjwa ya fizi na taya (Kiseyeye) hasahasa kwa watoto wadogo.Mpe mwanao kirutubisho hiki kwa kumkinga dhidi ya ugonjwa huu.Tunda la pera lina 120mg za vitamini C ambayo kwa mwanaume ni 90mg huhitajika kila siku na 75mg ambazo huhitajika kwa mwanamke.Faida nyingine ya kirutubisho hiki ni pamoja na kusaidia katika utengenezaji wa tishu mpya mwilini na kuchochea ufyonzaji wa chakula kilicho sagwa vyema mwilini,kwa kutokula pera na kukosa vitu hivi utaona ni kwa kiasi gani unakosa vitu muhimu.

MATATIZO YA UZAZI KWA WANAWAKE.
 Kuna kirutubisho kimoja aina ya FOLATE ambacho hupatikana ndani ya tunda hili la pera kinachofanya mayai ya mwanamke kukua vyema.Licha ya kuwa na tatizo la homoni za uzazi mwilini mwa mwanamke,anaweza kukabiliana na tatizo hilo kwa kutumia tunda la pera kama dawa ya tatizo lake na matokeo atayapata.Kwa dada mwenye matatizo ya uzazi kama kushindwa kuona siku zake na hata yule anayeshindwa kubeba mimba,kuna siri kubwa imefichika katika matumizi ya matunda siyo pera tuu bali hata na matunda mengine.kirutubisho hicho kina kazi nyingi zihusianazo na uzazi hivyo unaombwa kutumia tunda hilo kwaajili ya kuondokana na matatizo yasiyo ya lazima.

HUPUMZISHA MWILI.
 Uwepo wa vitamini B3 na B6 kunafanya mwili kuwa mtulivu na wenye mwendokasi uliotulia zaidi.Nakushauri baada ya kazi na uchovu wa mwili kula pera kwa ajili ya kuuburudisha mwili na kukufanya utulie kwa utulivu sahihi.Watafiti wanadai kuwa pera huuupa ubongo afya njema na mtulizo wa akili ulio sahihi na kuwa kufanya hivi huongeza uwezo wa utendaji kazi wa akili ya mtu,ukimwanzishia mwanao leo hii lishe sahihi ya tunda hili utamfanya kuwa na akili njema na ukuaji wake utasawijika kwani ni ubongo huo huo unaoooooorekebisha masuala ya ukuaji.

MATATIZO YA CHOO.
 Kamba lishe zilizopo ndani ya tunda hili zina mchango mkubwa sana katika kurekebisha matatizo ya choo,kwa wale wote wanaopata choo kigumu wanaweza wakaanza kutumia mapera kama njia mbadala ya kutibu tatizo lao.Pia kama una kumbukumbu nzuri utaona kwenye kila aina ya tunda tuliloliona mwanzo lina mchango mkubwa sana wa suala kama hili hivyo yunaweza kusema kwamba matunda yanatusaidia sana kukabiliana na tatizo hili.Kazi kubwa ya kambalishe hizi ni kusaidia usagaji wa chakula mwilini na ufyonzwaji wa maji katika sehemu ya mwisho ya usagaji yaani kwenye utumbo mkubwa.

DAWA YA TUMBO.
 Hapa ifahamike wazi kwamba majani ya mti wa mpera yana mchango mkubwa sana katika kutibu tumbo lolote lile liwe la kuhara au kuuma kwa kawaida.Sio dawa yenye masharti wala haikuhitaji kulipia hata gharama zaidi ya muda wako tuu,unashauriwa kuchukua majani machanga ya mpera na unaweza ukayatafuna bada ya kuyaosha au ukayachemsha kwa muda wa dakika kumi na ukanywa maji yake hayo kwa kipimo sahihi (usisubiri yapoe).

MZUNGUKO WA DAMU.
 Kutokana na kiasi kikubwa cha madini ya mangenese na iron iliyopo ndani ya tunda hili ni mchango mkubwa katika utengenezaji wa damu kwani madini ya chuma ndiyo hasa yanahitajika kwaajili ya kutengeneza damu.Uwepo wa madini haya mwilini kutokana na ulaji wa mapera utakuwezesha kukufanya uwe na utajiri mwingi wa damu na kuondoa matatizo yote yatokanayo na upungufu wa damu.
Pera pia lina kiasi kikubwa sana cha FOLIC acid ambayo ndiyo hitaji kuu la utengenezwaji wa damu ukitilia ndani madini ya iron.Asidi hii husaidia kuzuia ugonjwa wa anaemia kwani ndio ugonjwa mmojawapo utokanao na uchache wa damu mwilini.

  Antioxidant (kiondoa sumu) kilichomo ndani ya pera kina kazi muhimu san aya kutibu na kuondoa bacteria wasiohitajika tumboni,baadhi ya bacteria waliopo tumboni huzaliana kwa wingi na kusababisha hata UTI kwa wanawake.Si hayo tuu bali na magonjwa mengi kama kichwa kuuma,miguu na hata kuhara pia huondolewa kwa ulaji wa tunda hili,chukua maamuzi sahihi kama unaijali afya yako sasa.
   Anza sasa na usisubiri kwa ni bado hujachelewa,fuata kanuni sahihi za lishe ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya lazima uwe na afya bora.
Kwa maelezo,maswali na ushauri kuhusiana na afya yako usisite kuwasiliana nasi kwani tupo kwaajili ya kukufahamisha na kuhakikisha tuna share kile tunachokijua nawe pia ufaidike...Ahsante

PHONE: 0673666791

Email: goldamplat@gmail.com