Ijumaa, 18 Agosti 2017

KOMAMANGA .


        Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala haya,nakukaribisha tena ili kufahamu umuhimu wa tunda lingine aina ya Komamanga (POMEGRANATE kama waingereza wanavyoliita tunda hili).Ni tunda la tofauti kidogo kati ya matunda mengine ambayo tumekwisha yaona hapo awali kwani lina uwezo mkubwa sana ukilinganisha na matunda mengine,linatumika kutengenezea madawa ya aina mbalimbali ambayo hutumika katika vituo vya afya.Dawa hizo ni kama vile Tannis (punicalin na punicalagin), Flavonoids, Alkaloids, Steroids, Triterpenes na Polyphenols. Dawa hizi hupatikana katika magome, majani, mbegu, maganda ya matunda, juisi ya matunda na katika maua ya mkomamanga. Tunda la komamanga pia lina vitamini C na E kwa wingi amabazo tumeona mwanzoni kuwa na kazi kubwa kama kupambana na sumu mwilini (anti-oxidant) na kuharakisha uponaji wa vidonda (vitamin C) pamoaja na madini ya potassium na copper.

             Kihistoria tunda hili linajulikana sana na watu wa mashariki ya kati (middle east) kwani limetajwa sana katika vitabu vya dini kama tunda lenye uwezo mkubwa na lililopendwa na watu wenye hekima.Moja kati ya kazi kubwa inayofanywa na tunda hili ni pamoja na kuzuia kasi ya uzalianaji na ukuaji wa virusi vya UKIMWI,hivyo kupelekea tunda hili kuaminika kwa kupunguza kasi ya ukimwi kwa wale waathirika na ugonjwa huo.
  Utafiti huu ulichapishwa katika jarida la kisayansi la BMC infectious diseases (4) 41-45(2004). Matokeo yanayofanana na hayo pia yalithibitika katika utafiti mwingine uliofanywa na Kun Silprasit na wenzake mnamo mwaka wa 2011 na kupewa jina la “Anti-HIV-1 Reverse transcriptase activities of hexane extracts from Asian Medicinal Plants”. Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la kisayansi la “Journal of Medical Plant Research Vol. 5 (17), pp. 4194-4201, 9 Sept 2011”.
   Tunda hili linaaminika kuwa na kazi nyingi ikilinganishwa na matunda mengine na limejizolea umaarufu kulingana na uwezo wake mkubwa katika kupambana na ugonjwa huu mkubwa.Tuangalie faida zingine za kiafya zitokanazo na tunda hili la Komamanga.

TUMBO KUJAA GESI
  Vyakula tunavyokula vinazalisha gesi tumboni wakati wa kusagwa kwake,vyakula vya jamii ya mikunde hasahasa.Hii hupelekea tumbo kuunguruma mara kwa mara na kujihisi kushiba muda mwingi,ingawa siyo hali ya kawaida  na watu wengi wanalichukulia jambo hili kama ni kitu cha kawaida.Tumia majani ya komamanga kwa kuyachemsha na kunywa maji yake angalau mara mbili kwa siku kila baada ya mlo wako.

KUHARA DAMU.

  Bakteria ndani ya tumbo husababisha vidonda katika ukuta wa tumbo ambavyo huchelewa sana kupona na huvujisha damu ndani kwa ndani (haemorrhage),bakteria hao ni kama vile H.Pyroli na wengineo.Kwa kuwa tunda hili lina uwezo mkubwa katika kupambana na bakteria na virusi vya aina mbali mbali ndani ya mwili wa binadamu,ukitumia kwa muda mrefu linaweza kumaliza kabisa tatizo hilo.

KUDHIBITI TINDIKALI TUMBONI.

  Mchanganyiko wa madini yanayopatikana ndani ya tunda hili huzuia hali ya asidi tumboni (neutralization) na kusababisha utulivu kama ulikua na vidonda vya tumbo.tumia juisi (angalau glasi moja) kila baada ya mlo wa mchana.

KIHARUSI/STROKE.

  Huu ni ugonjwa wa kupooza kwa mwili unaotokana na kudhohofu kwa mishipa ya damu inayolishia ubongo.Kwakuwa tunda hili lina uwezo mkubwa wa kupambana na hali yoyote ya shambulio katuka damu na tunaona kwamba visababishi vya kiharusi kama vile sukari nyingi kwenye damu ambayo husababishwa na obesity,shambulio la wadudu/bakteria katika damu,vinaweza kuzuiliwa na tunda hili la komamanga.Nakushauri pendelea kutumia tunda hili kwa manufaa mbalimbali na siyo ulitumie kwa bahati mbaya.

MAGONJWA YA NYAMA ZA MOYO.

    Madini aina ya pottasium yanayopatikana ndani ya tunda hili yana faida kubwa sana ya kuimarisha uimara wa misuli na kukufanya uwe na misuli yenye nguvu pia.Hii itakupelekea kuondokana na tatizo la kuuma kwa misuli ya moyo ambayo mara nyingi humpata mtu ambaye hafanyi mazoezi mara kwa mara na kuufanya moyo wake kuwa mdhaifu.

TATIZO LA UNENE (OBESITY).

  Kama tulivyoona hapo juu kwamba kuongezeka kwa unene yaani Obesity kunasababishwa na mambo mengi kama kuongezeka kwa sukari ndani damu.Tatizo hili linaweza kuondoshwa kwa utumiaji wa tunda hili kwani lina sukari rahisi ambayo mmengenyo wake huwa nia rahisi ikilinganishwa na sukari inayopatikana ndani ya nafaka kama mahindi na mchele.Utaona wazi katika kutatua tatizo hili pia tatizo la kisukari litakukalia mbali na maisha yako daima.

Ukijilinganisha kiafya kati ya wewe na mtumiaji wa tunda la komamanga utaona tofauti kubwa sana kati yenu,kwani baadhi ya magonjwa ambayo yanakusumbua wewe mara kwa mara mwenzako atakwambia hayajawahi kumpata huu ni mwaka wa tano au sita.Ndipo utakapogundua umuhimu wa kutumia tunda hili.
 Kuna madhara ya kutumia tunda hili kwa wingi,kwani kama tunavyojua kwamba kila kitu ukizidisha kuna madhara utakayoyapata,pia hata ukizidisha dozi ya tunda hili kuna madhara ambayo utakayoyapata na madhara hayo ni kama ifuatavyo;
               Madhara yanayoweza kutokea kwa kutumia dawa-lishe hii (Adverse reactions)
Matumizi ya kipimo kikubwa cha dawa hii ikiwa katika hali yake ya asili (zaidi ya gram 80) kinaweza kusababisha kizunguzungu, maumivu makali ya kichwa, kushindwa kufumbua macho, kutapika, kuzimia na wakati mwingine inaweza kusababisha kifo. Dawa hii pia inaweza kusababisha mwili kunyong’onyea, kutokuona vizuri, kushitukashituka kwa misuli na kutetemeka kwa mikono kama mlevi (tremors).

                                PHONE:   0673666791 
                                Email: goldamplat@gmail.com


     Kwa swali lolote kuhusiana na afya yako usisite kuuliza.
      JENGA AFYA YAKO NA AMPLAT-AFYA KWANZA