Jumatano, 18 Januari 2017

FENESI.

   Kama ilivyo ada ni wasaha mwingine ambao tunamshukuru mungu kwa kutupa uzima na kukutana tena katika makala yetu ya kila siku.Tunapaswa kumshukuru mungu kwani bila yeye hakuna ambalo tunalifanya na kuwa sahihi
Leo nitakupeleka moja kwa moja kuona umuhimu wa tunda aina ya fenesi kiafya ya ndani na nje ya mwili.
 
    Tunda la fenesi ni moja kati ya matunda yenye sukari kwa kiasi chake,ulaji wa 100g za fenesi hukupa karolizi 90 kutokana sukari aina ya fructose na sucrose zilizomo ndani ya tunda hili.Kutokana na ukweli kwamba matunda mengi huwa na virutubisho vingi vinavyofanana hasa vitamini C,utaona kazi nyingi za baadhi ya matunda pia hufanana.Tuangalie faida za tunda hili kiafya kama ilivyo kawaida yetu:

MAGONJWA YA MOYO.
Sababu mojawapo ya magonjwa ya moyo ni pamoja na sukari kuwepo kwa wingi ndani ya mzunguko wa damu hii husababisha kuongezeka kwa kasi ya usafirishaji wa damu na mapigo ya moyo (blood pressure).Hii hupunguzwa kutokana na tunda la fenesi kuwa na kiwango cha sukari ambayo husaidia kurekebisha sukari mwilini.Hata hivyo mafuta yapatikanayo ndani ya fenesi hayana lehemu,hivyo ni mafuta sahii kutumika na yana uwezo mkubwa wa kukabiliana na tatizo la pressure hasa ya kupanda.
 
HUTIBU TATIZO LA DAMU.
Uwepo wa potasium na baadhi ya madini kama folic acid ndani ya tunda hili husaidia kwa kiasi kikubwa kusulihisha suala la damu.Kwa kuwa na anti oxidant Fenesi husaidia kuondoa sumu mwilini na kukupunguzia kasi ya magonjwa ya kansa na kulipunguzia ini kazi nzito ya kupambana na sumu mwilini.

MIFUPA NA MENO.
Mifupa huwa dhaifu kutokana na umri,vyakula tunavyokula pamoja na maradhi lakini vyote hivyo huweza kuepukika kama utaamua kuanza leo afya lishe na tunda hili.Fenesi lina madini mengi ya magnesium na kalisium ambayo husaidia kwa kiasi fulani katika kuimarisha mifupa.Hata magonjwa ya meno hutibiwa kwa fenesi kwani lina kiwango kikubwa cha vitamini Cambayo hufanya kazi nzuri katika kuimarisha uimara wa meno.
 
HULINDA NGOZI.
Dawa sahihi ya ngozi zilizojikunja (kama za wazee) ni Fenesi,hii ni kutokana na kiasi kikubwa cha mafuta ambacho tunda hili kinacho ambacho husaidia katika kulainisha ngozi na kuipa muonekano mwaroro.Sio hadithi za dhahania bali ni ukweli kwamba mafuta ya ngozi yatokanayo na fenesi ndio yaliyothibitishwa kuwa mafuta bora kwa afya ya ngozi ya binadamu.Fenesi huipa ngozi mwonekano kama wa ngozi ya mtoto mdogo,hivyo kwa akina dada si vyema sana kuhangaika na vipodozi vyenye madhara na gharama kubwa bali ubadilishe mazoea na kuanza kutumia fenesi kwa uzuri wa ngozi yako.
 
UNG"AAVU WA MBONI ZA MACHO.
Kutokana na uwepo wa vitamini A ambayo kazi yake kubwa ni kuyafanya macho yawe na uwezo mzuri wa kuona,pia hupatikana ndani ya tunda hili nakufanya kuwa na kazi muhimu ambayo inahitajika kila siku kwani tatizo la macho kwa kiasi kikubwa huathiri mwenendo mzima wa maisha yetu ya kila siku.
      Ulaji wowote uliopitiliza ni hatari kwa afya yako hata kama kitu hicho kitakua na faida mara mia,unatakiwa kula kistaarabu na kwa kiasi na sio kwamba umejua kuna faida za kutumia chakula hicho ukatumia zaidi.Mchanganyo wa fenesi na vyakula vingine huleta sumu ndani ya mwili wako,kaa na taadhari
 ONYO: USIJARIBU KULA FENESI NA KUNYWA SODA YA COCOA-COLA KWA MFUATANO.
 Kufanya hivyo unahatarisha maisha yako kwa muda mchache sana,kwani mchanganyiko huo husababisha utengenezwaji wa sumu ifananayo na nyoka aina ya cobra.
Utafitii uliofanyika china umedhihirisha jambo hilo:

 Kwa mapendekezo,maoni,maswali na ushauri wowote  juu ya tatizo lolote kuhusiana na AFYA usisite kuwasiliana nasi muda wowote.
PHONE:        0673666791


Jumanne, 17 Januari 2017

NANASI.

 

     Leo tena katika makala nyingine tunakutana kuzungumzia tunda aina ya nanasi,kabla ya kuanza mada yetu hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea na kutuweka salama mpaka muda huu.Ni matumaini yangu ni wazima wa afya na mmejaaliwa kuiona siku nyingine hivyo sifa na utukufu arudishiwe Mungu muweza yote.
   Nanasi kama linavyojulikana kwa jina lingine la Pineapple ni tunda linalopendwa na watoto wengi kwani lina sukari nyingi ukilinganisha na matunda mengine.Licha ya watoto pia hata watu wazima wanapenda sana juisi ya nanasi kutokana na utamu wa ladha iliyokua nayo.Tunda hili ni miongoni mwa matunda yanayoongoza kutibu magonjwa ya koo na yamekuwa yakitumika na wengi kutokana na kazi hii.Baada ya kumenywa vizuri na kuwa tayari kwa kuliwa,nanasi halitakiwi kuhifadhiwa ndani ya friji kwani hupoteza ubora wa virutubisho vyake bali kwa kuliweka katika chombo chenye mfuniko na kulihifadhi vizuri hulipa thamani yake sahihi hata kwa muda wa zaidi ya siku nne.
   Kama yalivyo matunda mengine,nanasi linaweza kuliwa kama jinsi lilivyo au likatengenezewa juisi,njia zote ni sahihi katika kupata virutubisho sahihi vya tunda hili.Tuangalie umuhimu wake katika kutibu na kuzuia baadhi ya magonjwa;

MAGONJWA YA KOO.
 Tunda hili limeonekana kuweza kupambana na ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo

MAGONJWA YA TUMBO.
 Udhaifu wa tumbo kushindwa kusaga chakula hasa protini hurekebishwa na tunda la nanasi.Hii ni kutokana na uwepo wa kimeng"enya cha aina ya Bromelain ambacho hufanya kazi kubwa ya kusaidia kusaga vyakula vilivyo na ugumu katika usagaji wake.Hii hupelekea tatizo hilo kutatuliwa na tunda hili hivyo kulifanya kuaminika na watu wengi katika kutatua tatizo hilo.

KULAINISHA CHOO.
 Kamba lishe zilizomo ndani ya papai husaidia tatizo la choo na kutoa choo laini na sio kigumu.Kwakua nanasi lina majimaji kwa kiasi kingi huweza kuzuia tatizo la uhaba wa maji katika mfumo wa chakula mwilini mwa binadamu.Kwa ushauri wa tatizo hili tumia nanasi na uone mafanikio sasa

HUONGEZA DAMU.
 Nanasi lina kiasi fulani cha madini chuma ambayo husaidia katika kuongeza damu kwani huusika na utengenezaji wa damu mwilini mwa binadamu.wagonjwa wengi waliopungukiwa na damu hushauriwa kutumia tunda hili kaam njia mbadala ya kuongeza damu mwilini mwao.
 

BARIDI YABISI (ATHRITIS).
 Baadhi ya magonjwa ya baridi yabisi yaani magonjwa ya jointi hutatuiliwa kwa ulaji wa nanasi kutokana na uwingi wa vitamini zilizomo kwenye tunda hili kama vile vitamini A,B, na C.Wazee wengi huwa na tatizo hili hivyo hushauriwa kutumia nanasi kwa kutatua tatizo hili.

     Uwepo wa vitamini hizo husaidia kukabiliana na magonjwa mengine kama ya fizi,meno na magonjwa mengine ya mifupa na sio magonjwa machache niliyoyaelezea hapo juu tuu bali na mengine ambayo tutazidi kuelezana kadri tunavyokua pamoja.

     Kuna dhana inayosikika kwamba nanasi si tunda bora kwa akina mama wajawazito kwani huwaletea matatizo,jambo hilo sio la kweli na ni kama hadithi zilizo simuliwa zamani za mababu zetu za kukataza mama mjamzito kutumia baadhi ya vyakula fulani.
Tumia nanasi ukiwa na lengo la kuboresha na kuimarisha afya yako na sio kwa mazoea ya kula ilimradi umekula.
   Fuata kanuni na taratibu sahihi za afya kwa matokeo sahihi ya afya bora na sio kufanya kwa mazoea,mfundishe mwanao,rafiki na hata jirani yako juu ya umuhimu wa tunda hili naye anufaike.
Kwa mtazamo na maoni yoyote juu ya jambo lolote lihusianalo na afya yako usisite kuwasiliana nasi kwa namba hapo chini,Ahsante.

  PHONE; 0673666791
  Email; goldamplat@mail.com

Jumatatu, 16 Januari 2017

MACHUNGWA


        Habari ndugu msomaji ni matumaini yangu u mzima wa afya na Mungu amekujal;ia afya iliyo imara,kama ni mgonjwa pia unatakiwa kumshukuru mungu na kuangalia wapi ulikosea kufuata kanuni za afya na ujirekebishe ili kurudia katika hali yako ya uzima.
Leo tutaangalia umuhimu wa tunda aina ya Chungwa kwani wengi wamekua wakiniuliza baadhi ya maswali kuhusiana na tunda hili.
    Kwanza kabisa tunda hili halitakiwi kuliwa na mtu mwenye vidonda vya tumbo kama hajala kitu chochote kwani ni aina ya tunda lenye asidi ambayo inaweza ikamletea matatizo katika vidonda vyake.Pia mbegu za tunda hili licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini,vitamini na madini mengine,zinz kiwango kikubwa cha sumu aina ya Cynide (sayanid) ambayo kama itapatikana kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu ni sumu ambayo inaweza kuua kwa haraka.
 Faida za virutubisho ambavyo vipo ndani ya chungwa hupatikana katika sehemu kuu mbili nazo ni Maji ya chungwa (mchuzi wa chungwa) na kwenye nyama ya chungwa.Unashauriwa kula chungwa lote na sio kukamua maji yake na kisha kulitupa kwani utakosa kambalishe zipatikanazo kwenye nyama ya chungwa.Watoto wadogo hufanya hivyo mara nyingi,sio inamaanisha wanakosa virutubisho vyote hapana! bali wanapata vichache vile vilivyomo ndani ya mchuzi pekee.
 Hivyo na kwa wewe ambae ulikua huafahamu jambo hilo sasa umelifahamu na nina imani utabadilika na kulifanyia kazi kwa manufaa ya afya yako mwenyewe.
   Hata hivyo licha ya yote hayo bado tunaona tunda hili lina faida mbalimbali mwilini kama vile;

UKOSEFU WA CHOO.
 Uwepo wa kambalishe ndani ya tunda hili husaidia katika usagaji wa chakula na kuondoa kabisa tatizo la choo.Pia kolesto zilizopo mwilini hupungua kwani umuhimu wa kambalishe hizi huonekana katika usagaji wa chakula na kusababisha mafuta yote yaliyozidi mwilini kutumika kwa kuyeyushwa na hivyo kufanya tatizo hili lisiwepo kabisa.
 
MAGONJWA YA MOYO.
 Flavonoidi pamoja na vitamini C inatopatikana ndani ya tunda hili husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kama vile mafuta kujaa ndani ya mishipa ya moyo kama tulivyoona hapo juu.
 
MAGONJWA YA MENO NA FIZI.
 Uwepo wa vitamini C ambayo husaidia katika kupambana na magonjwa ya udhaifu wa meno na fizi,utakusaidia katika kuimarisha afya ya meno na fizi zako kwa ujumla.

MAGONJWA YA MAPAFU.
 Chungwa lina kiasi kikubwa cha vitamini B6 na madini ya chuma ambayo husaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu ambazo huusika na usafirishaji wa hewa safi mwilini.Hii huondoa matatizo ya mapafu na mzunguko wa hewa safi mwilini moja kwa moja.

SHINIKIZO LA DAMU.
 Machungwa ni muhimu kwa wagonjwa wenye shinikizo kubwa la damu (presha) kwani kwa kuondoa mafuta yaliyorundikana kwanye mishipa ya damu pamoja na kuwa na virutubisho vya magnesium huondoa kabisa tatizo hili na kufanya mwenye tatizo kama hilo kupona na kujisikia vyema.
   Si mpaka uwe mgonjwa ndio uanze kutumia machungwa na matunda mengine bali kinga ni bora kuliko tiba.Ni bora kujiwekea mazoea ya kula matunda kwa wingi ili kupata virutubisho vinavyohitajika vikawe kama akiba ya baadae na kinga kwa magonjwa nyemelezi.

MAGONJWA YA FIGO.
 Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kurekebisha Ph ambayo itakufanya uwe na hali iliyo timilifu ndani ya mwili wako hii hulipumzisha ini pamoja na figo katika kufanya kazi nzito ya kurekebisha na kupambana na hali inayobadilika mara kwa mara.
 
KUONDOA CHOLESTEROL.
 Uwepo wa kirutubisho cha lemonin ndani ya machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa sana kuondoa mafuta ambayo hayahitajiki ndani ya miili yetu.Hasahasa kwa watu wanene kupita kiasi (obese) wanaweza wakapunguza unene huo kwa kufuata utaratibu wa matumizi bora na sahihi ya matunda kama machungwa na mengineyo.

   Ulaji wa chungwa pia umetofautiana kama tulivyoona hapo juu,hivyo unaweza ukaamua wewe utumie tunda hili kama juisi au kama tunda la kawaida kulila.Na pia ulaji wake tumeuangalia hapo juu hivyo nakushauri uache kula kwa mazoea, na uanze kula kwa faida ya afya na sio ladha pekee.
Kwa ushauri na tatizo lolote linalohusiana na afya yako usisite kuwasiliana nasi muda wowote na pia kama una maoni,ushauri na vyovyote uonavyo wewe wasilisha kwa mawasiliano yetu hapo chini.Mungu akubariki.

    PHONE: 0673666791

    Email: goldamplat@mail.com

                www.amplatblogspot.com