Jumanne, 17 Januari 2017

NANASI.

 

     Leo tena katika makala nyingine tunakutana kuzungumzia tunda aina ya nanasi,kabla ya kuanza mada yetu hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea na kutuweka salama mpaka muda huu.Ni matumaini yangu ni wazima wa afya na mmejaaliwa kuiona siku nyingine hivyo sifa na utukufu arudishiwe Mungu muweza yote.
   Nanasi kama linavyojulikana kwa jina lingine la Pineapple ni tunda linalopendwa na watoto wengi kwani lina sukari nyingi ukilinganisha na matunda mengine.Licha ya watoto pia hata watu wazima wanapenda sana juisi ya nanasi kutokana na utamu wa ladha iliyokua nayo.Tunda hili ni miongoni mwa matunda yanayoongoza kutibu magonjwa ya koo na yamekuwa yakitumika na wengi kutokana na kazi hii.Baada ya kumenywa vizuri na kuwa tayari kwa kuliwa,nanasi halitakiwi kuhifadhiwa ndani ya friji kwani hupoteza ubora wa virutubisho vyake bali kwa kuliweka katika chombo chenye mfuniko na kulihifadhi vizuri hulipa thamani yake sahihi hata kwa muda wa zaidi ya siku nne.
   Kama yalivyo matunda mengine,nanasi linaweza kuliwa kama jinsi lilivyo au likatengenezewa juisi,njia zote ni sahihi katika kupata virutubisho sahihi vya tunda hili.Tuangalie umuhimu wake katika kutibu na kuzuia baadhi ya magonjwa;

MAGONJWA YA KOO.
 Tunda hili limeonekana kuweza kupambana na ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo

MAGONJWA YA TUMBO.
 Udhaifu wa tumbo kushindwa kusaga chakula hasa protini hurekebishwa na tunda la nanasi.Hii ni kutokana na uwepo wa kimeng"enya cha aina ya Bromelain ambacho hufanya kazi kubwa ya kusaidia kusaga vyakula vilivyo na ugumu katika usagaji wake.Hii hupelekea tatizo hilo kutatuliwa na tunda hili hivyo kulifanya kuaminika na watu wengi katika kutatua tatizo hilo.

KULAINISHA CHOO.
 Kamba lishe zilizomo ndani ya papai husaidia tatizo la choo na kutoa choo laini na sio kigumu.Kwakua nanasi lina majimaji kwa kiasi kingi huweza kuzuia tatizo la uhaba wa maji katika mfumo wa chakula mwilini mwa binadamu.Kwa ushauri wa tatizo hili tumia nanasi na uone mafanikio sasa

HUONGEZA DAMU.
 Nanasi lina kiasi fulani cha madini chuma ambayo husaidia katika kuongeza damu kwani huusika na utengenezaji wa damu mwilini mwa binadamu.wagonjwa wengi waliopungukiwa na damu hushauriwa kutumia tunda hili kaam njia mbadala ya kuongeza damu mwilini mwao.
 

BARIDI YABISI (ATHRITIS).
 Baadhi ya magonjwa ya baridi yabisi yaani magonjwa ya jointi hutatuiliwa kwa ulaji wa nanasi kutokana na uwingi wa vitamini zilizomo kwenye tunda hili kama vile vitamini A,B, na C.Wazee wengi huwa na tatizo hili hivyo hushauriwa kutumia nanasi kwa kutatua tatizo hili.

     Uwepo wa vitamini hizo husaidia kukabiliana na magonjwa mengine kama ya fizi,meno na magonjwa mengine ya mifupa na sio magonjwa machache niliyoyaelezea hapo juu tuu bali na mengine ambayo tutazidi kuelezana kadri tunavyokua pamoja.

     Kuna dhana inayosikika kwamba nanasi si tunda bora kwa akina mama wajawazito kwani huwaletea matatizo,jambo hilo sio la kweli na ni kama hadithi zilizo simuliwa zamani za mababu zetu za kukataza mama mjamzito kutumia baadhi ya vyakula fulani.
Tumia nanasi ukiwa na lengo la kuboresha na kuimarisha afya yako na sio kwa mazoea ya kula ilimradi umekula.
   Fuata kanuni na taratibu sahihi za afya kwa matokeo sahihi ya afya bora na sio kufanya kwa mazoea,mfundishe mwanao,rafiki na hata jirani yako juu ya umuhimu wa tunda hili naye anufaike.
Kwa mtazamo na maoni yoyote juu ya jambo lolote lihusianalo na afya yako usisite kuwasiliana nasi kwa namba hapo chini,Ahsante.

  PHONE; 0673666791
  Email; goldamplat@mail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni