Jumatatu, 16 Januari 2017

MACHUNGWA


        Habari ndugu msomaji ni matumaini yangu u mzima wa afya na Mungu amekujal;ia afya iliyo imara,kama ni mgonjwa pia unatakiwa kumshukuru mungu na kuangalia wapi ulikosea kufuata kanuni za afya na ujirekebishe ili kurudia katika hali yako ya uzima.
Leo tutaangalia umuhimu wa tunda aina ya Chungwa kwani wengi wamekua wakiniuliza baadhi ya maswali kuhusiana na tunda hili.
    Kwanza kabisa tunda hili halitakiwi kuliwa na mtu mwenye vidonda vya tumbo kama hajala kitu chochote kwani ni aina ya tunda lenye asidi ambayo inaweza ikamletea matatizo katika vidonda vyake.Pia mbegu za tunda hili licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini,vitamini na madini mengine,zinz kiwango kikubwa cha sumu aina ya Cynide (sayanid) ambayo kama itapatikana kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu ni sumu ambayo inaweza kuua kwa haraka.
 Faida za virutubisho ambavyo vipo ndani ya chungwa hupatikana katika sehemu kuu mbili nazo ni Maji ya chungwa (mchuzi wa chungwa) na kwenye nyama ya chungwa.Unashauriwa kula chungwa lote na sio kukamua maji yake na kisha kulitupa kwani utakosa kambalishe zipatikanazo kwenye nyama ya chungwa.Watoto wadogo hufanya hivyo mara nyingi,sio inamaanisha wanakosa virutubisho vyote hapana! bali wanapata vichache vile vilivyomo ndani ya mchuzi pekee.
 Hivyo na kwa wewe ambae ulikua huafahamu jambo hilo sasa umelifahamu na nina imani utabadilika na kulifanyia kazi kwa manufaa ya afya yako mwenyewe.
   Hata hivyo licha ya yote hayo bado tunaona tunda hili lina faida mbalimbali mwilini kama vile;

UKOSEFU WA CHOO.
 Uwepo wa kambalishe ndani ya tunda hili husaidia katika usagaji wa chakula na kuondoa kabisa tatizo la choo.Pia kolesto zilizopo mwilini hupungua kwani umuhimu wa kambalishe hizi huonekana katika usagaji wa chakula na kusababisha mafuta yote yaliyozidi mwilini kutumika kwa kuyeyushwa na hivyo kufanya tatizo hili lisiwepo kabisa.
 
MAGONJWA YA MOYO.
 Flavonoidi pamoja na vitamini C inatopatikana ndani ya tunda hili husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kama vile mafuta kujaa ndani ya mishipa ya moyo kama tulivyoona hapo juu.
 
MAGONJWA YA MENO NA FIZI.
 Uwepo wa vitamini C ambayo husaidia katika kupambana na magonjwa ya udhaifu wa meno na fizi,utakusaidia katika kuimarisha afya ya meno na fizi zako kwa ujumla.

MAGONJWA YA MAPAFU.
 Chungwa lina kiasi kikubwa cha vitamini B6 na madini ya chuma ambayo husaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu ambazo huusika na usafirishaji wa hewa safi mwilini.Hii huondoa matatizo ya mapafu na mzunguko wa hewa safi mwilini moja kwa moja.

SHINIKIZO LA DAMU.
 Machungwa ni muhimu kwa wagonjwa wenye shinikizo kubwa la damu (presha) kwani kwa kuondoa mafuta yaliyorundikana kwanye mishipa ya damu pamoja na kuwa na virutubisho vya magnesium huondoa kabisa tatizo hili na kufanya mwenye tatizo kama hilo kupona na kujisikia vyema.
   Si mpaka uwe mgonjwa ndio uanze kutumia machungwa na matunda mengine bali kinga ni bora kuliko tiba.Ni bora kujiwekea mazoea ya kula matunda kwa wingi ili kupata virutubisho vinavyohitajika vikawe kama akiba ya baadae na kinga kwa magonjwa nyemelezi.

MAGONJWA YA FIGO.
 Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kurekebisha Ph ambayo itakufanya uwe na hali iliyo timilifu ndani ya mwili wako hii hulipumzisha ini pamoja na figo katika kufanya kazi nzito ya kurekebisha na kupambana na hali inayobadilika mara kwa mara.
 
KUONDOA CHOLESTEROL.
 Uwepo wa kirutubisho cha lemonin ndani ya machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa sana kuondoa mafuta ambayo hayahitajiki ndani ya miili yetu.Hasahasa kwa watu wanene kupita kiasi (obese) wanaweza wakapunguza unene huo kwa kufuata utaratibu wa matumizi bora na sahihi ya matunda kama machungwa na mengineyo.

   Ulaji wa chungwa pia umetofautiana kama tulivyoona hapo juu,hivyo unaweza ukaamua wewe utumie tunda hili kama juisi au kama tunda la kawaida kulila.Na pia ulaji wake tumeuangalia hapo juu hivyo nakushauri uache kula kwa mazoea, na uanze kula kwa faida ya afya na sio ladha pekee.
Kwa ushauri na tatizo lolote linalohusiana na afya yako usisite kuwasiliana nasi muda wowote na pia kama una maoni,ushauri na vyovyote uonavyo wewe wasilisha kwa mawasiliano yetu hapo chini.Mungu akubariki.

    PHONE: 0673666791

    Email: goldamplat@mail.com

                www.amplatblogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni