Jumatatu, 30 Januari 2017

  UKWAJU.


    Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala haya,nakukaribisha tena ili kufahamu umuhimu wa tunda lingine aina ya Ukwaju.Ni tunda la tofauti kidogo kati ya matunda mengine ambayo tumekwisha yaona hapo awali lakini leo ngoja tuangalie umuhimu wa utofauti wake na matunda mengine.

    Kidogo ni tunda la kushangaza kwani lina ladha tamu na chachu,tunda hili unapoanza kula kwanza lazima likusisimue ndipo uendano nalo na imekua ni vigumu kwa watoto wadogo kulila tunda hili wenyewe kama wenyewe kutokana na ladha yake.Ulaji wake haujatofautiana na matunda mengine kwani unaweza kulila kama tunda,ukatengeneza juisi na ukanywa na hata ukatumia kama siagi.Kusema kweli ni tunda lenye maana kubwa kutokana na kazi lilizokua nalo,tuangalie baadhi ya kazi hizo ni kama ifuatavyo.

HUTIBU HOMA.
 Kuanzia homa ya tumbo mpaka homa ya manjano tunda hili hutibu pasipo kuangalia.Hii ni kutokana na asidi liyopo ndani ya tunda hili inayozuia kabisa uzalianaji wa bacteria hatari ndani ya tumbo na kuwaacha wale wanaohitajika kubaki tuu.Imetumika kama dawa yenye manufaa zaidi kwani mtu akiumwa tumbo na kutumia ukwaju basi amejihakikishia pona yake.

HUSAIDIA USAGAJI WA CHAKULA.
 Kama yalivyo matunda mengine,ukwaju una nyuzi nyuzi ambazo husaidia katika usagaji wa chakula na kukupa choo kizuri kama tulivyoona katika matoleo ya nyuma.Kwa mwenye tatizo kama hili hatakiwi kuuliza afanye nini ili aweze kujiponya wakati dawa ya ukwaju tayari ipo na inapatikana sokoni.

HUTIBU VIDONDA.
 Vidonda vya kuungua hupona kwa kutumia ukwaju,lakini mara nyingi hutokana baada ya mchanganyiko wa tunda hili na asali.Mchanganyo utakaotumika kama dawa unatofautiana kulingana na sehemu ya jeraha au ukubwa wa jeraha pia.

HUTIBU MAAMBUKIZI YA KOO.
 Bakteria pamoja na protozoa wengine wanaoshambulia mfumo wa upumuaji huzuiwa kufanya hivyo mara tuu wanapotaka kuingia kwenye sehemu za ndani kabisa za mfumo huo kutokana na asidi inaypatikana ndani ya tunda hili,hii itakuweka huru na magonjwa yote ya koo na hata ya mfumo wa chakula kwani ni koo hilohilo ndilo linalounganisha mifumo hiyo miwili.

HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KANSA.
 Tunda la ukwaju limewasaidia wengi katika kurekebisha afya zao na kupunguza uwezekano mkubwa wa kupata kansa kwani ladha yake ya uchachu hairuhusu ukuaji wa kansa mwilini.Unashauriwa kutumia mara kwa mara ili kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata kansa mwilini mwako.Kinga za ukwaju zitazuia ukuaji wa kansa kama zitapatikana kwa wingi mwilini mwako na si vinginevyo.

UKOSEFU WA HAMU YA KULA.
 Kwa wale wanaokosa hamu ya kula chakula,tunda la ukwaju ni msaada mzuri kukurejesha katika hali yako madhubuti.Ingawa watoto wengi hukumbwa na tatizo hili pale ambapo wanakua au wamepatwa na homa,andaa juisi yako ya ukwaju na kisha tumia kikombe kimoja nusu saa kabla ya kula utaona mafanikio.

    kutokana na kazi hizo,tunashauri tunda la ukwaju lisikose katika mlo wako wa kila siku kwani lin kazi kubwa sana ukilinganisha na matunda mengine ingawa baadhi zinafanana.Tumia ukwaju kama dawa kama ninavyokwambia kwenye matunda mengine na sio utumie pale ambapo unaona tatizo limekufika kwani hata kama utapata mafanikio hayatakua makubwa kwani matunda mengi ni kinga dhidi ya magonjwa na machache ni dawa hivyo unapaswa kutumia kwa kujitaadharisha na magonjwa yajayo.

  Kama utakua unafanya hivyo kwa utaratibu wa kujiwekea ulinzi na akiba ya kinga mwilini utakua mbali kiafya na hautasumbuliwa na magonjwa nyemelezi kirahisi,lakini hakikisha unamshauri na ndugu au rafiki na hata mwenzako uliye nae jirani kufuata kanuni na taratibu za afya ili aepukane na magonjwa.
  Sina la ziada kwa siku ya leo,kwa maswali juu ya afya yako na ushauri wowote usisite kuwasiliana nasi tutakusaidia vyema kwa wakati wowote na muda wowote.Ahsante

Kwa mawasiliano usisite kututafuta;

  PHONE : 0673666791

  Email:  goldamplat@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni