Jumatano, 25 Januari 2017

KAROTI.


          Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala haya,nakukaribisha tena ili kufahamu umuhimu wa tunda lingine aina ya Karoti.Ni tunda la tofauti kidogo kati ya matunda mengine ambayo tumekwisha yaona hapo awali lakini leo ngoja tuangalie umuhimu wa utofauti wake na matunda mengine.
   Kwanza hili ni tunda pekee ambalo linaweza kupikwa na lisiharibu ladha yake,pia linaweza kuliwa likiwa kama matunda mengine yanavyoliwa bila kupikwa.Pia tunda hili ni moja wapo kati ya matunda machache ambayo yanaoatikana chini ya ardhi,tumezoea matunda mengi hupatikana juu ya miti au hata yakiwa yamelala ardhini lakini sio chini ya ardhi kwa kufanya kuyafukua/kuchimba.

  Kuna aina tatu za karoti ambazo hutofautiana kwa rangi zake,kuna karoti nyekundu,ya njano na ya pinki lakini zote ni karoti.Karoti za njano na nyekundu ndizo zenye virutubisho vingi ukilinganisha na hiyo ya pink na mara nyingi ndizo aina za karoti ambazo hulimwa sana nchini kwetu Tz.
    Karoti kama yalivyo matunda mengine lina faida kubwa sana nyingi,watu wengi tumekua tukisikia faida moja tuu ya kutibu macho na kuyafanya yawe maangavu.Ni kweli lakini siyo kazi hiyo tuu bali kuna kazi nyingi za aina mbalimbali,ungana nami tuzione hapo chini;

 HUTIBU MATATIZO YA CHOO.
  Karoti lina kiasi kikubwa cha kamba lishe ambazo ndizo muhimu katika kurekebisha tumbo na kukupatia choo kizuri.Kambalishe hizi husaidia katika ufyonzaji wa maji katika njia ya mwisho ya usagaji wa chakula hivyo kukuweka katika hali nzuri kama zitapatikana kwa kiasi kikubwa mwilini.

 HULAINISHA NGOZI.
  Kwa mtumiaji wa karoti mara kwa mara atakubaliana na mimi kwa kazi hii ambayo karoti inafanya,warembo wengi wanatumia mafuta na losheni za ngozi zilizotengenezwa na tunda hili kwaajili ya umakini wa ngozi zao.Hii inatokana na uwepo wa vitamini E iliyopo ndani ya karoti inayofanya kazi ya kurudisha na kutengeneza seli mpya za ngozi zilizo haribika/kufa.

 HUFANYA MACHO KUWA MAANGAVU.
  Karoti ina kirutubisho kiitwacho Beta-carotenene ambacho ndio chanzo muhimu cha vitamini A mwilini.Baada ya kubadilishwa na kuwa vitamini A mwilini,carotenene hupelekwa moja kwa moja katika utengenezaji wa seli ndani ya pupil na retina kwenye macho.Hii hufanya uwingi wa seli hizi na kusababisha kuondoa tatizo la kutokuona kwenye mwanga hafifu au mdogo.

 HUONDOA TATIZO LA CHUNUSI.
  Kama tulivyoona hapo juu vitamin E ndiyo hasa itumikayo kupambana na magonjwa ya ngozi,hivyo kwa uwepo wa vitamini hii hutatua tatizo la chunusi na vipele vitokanavyo na mafuta mengi usoni.

CHANZO CHA NISHATI MWILINI.
 Karoti haina mafuta bali ina karolies nyingi,hivyo kwa mtumiaji wa karati hupata virutubisho hivi kwa wingi na kumfanya awe na nguvu za kumwezesha kuhimili kazi mbalimbali.

 HUREKEBISHA TATIZO LA DAMU.
  Juisi ya karoti inasifika kurekebisha tatizo la upungufu wa damu mwilini,kwa matumizi ya kama dawa unashauriwa kutumia ndani ya muda wa si chini ya miezi mitatu.Kunywa glasi moja ya juisi kila siku kwa matatizo ya damu.

  Karoti ni muhimu sana kwa watoto wadogo kwani ina vitamini A nyingi ambazo zitamjengea mtoto kinga nzuri juu ya magonjwa mengine mengi tofauti na ya macho.Unashauriwa kumwanzishia mtoto wako mdogo utaratibu wa kunywa juisi ya karoti kama dawa kwa kumkinga na monjwa mengine mengi.
Tunda hili limekuwa na sifa nyingi kutokana na kazi yake kubwa moja ya kutibu macho.
   Kwa kuwa na viondoa sumu vingi ndani ya karoti,imekuwa na mchango mkubwa wa kutibu magonjwa ya kansa kama vile kansa ya mapafu,tumbo na tezi za uzazi za kiume.
Kwa faida nyingine nyingi tazama; http://www.a2ztube.co.
  Kwa lolote linakusumbua kuhusu afya yako usisite kuwasiliana nasi kwa ushauri na kukujibu maswali yako.Pia tunatoa huduma za kufundisha taratibu za milo mingine kwa ajili ya matatizo ya afya yatokanayo na mfumo wa maisha...Ahsante.

PHONE;  0673666791

Email: goldamplat@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni