Jumapili, 22 Januari 2017

 TIKITI-MAJI.



     Leo tena katika makala nyingine tunakutana kuzungumzia tunda aina ya Tikiti-maji,kabla ya kuanza mada yetu hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea na kutuweka salama mpaka muda huu.Ni matumaini yangu ni wazima wa afya na mmejaaliwa kuiona siku nyingine hivyo sifa na utukufu arudishiwe Mungu muweza yote.

  Kama wengi jinsi tunavyolifahamu tunda hili kuwa na uwingi wa 92% ya maji pekee ndivyo kazi yake kubwa yakuhakikisha maji mwilini mwa mtumiaji hayapungui.Tikiti-maji lina aina mbalimbalio za madini ambayo hufanya kazi nyingi mwilini mwetu na kusaidia kuboresha afya ya mlaji.
Tuangalie baadhi ya kazi muhimu za tunda hili;

HUONGEZA NGUVU ZA KIUME.
 Kila kipatikanacho ndani ya tunda hili kina kazi kubwa ukianzia majani,maganda pamoja na mbegu.Wanaume wengi wamekua wakikumbwa na tatizo la hili na kumekuwa na matangazo mbalimbali kuhusiana na dawa za kusaidia tatizo hili.Ndugu msomaji ni bora kutumia dawa za matunda/lishe ili kutibu au kupunguza au kuzuia tatizo lako na sio kila dawa kuiona inafaa.Mbegu za tunda hili zikiliwa pamoja na nyama ya tunda hili husaidia katika kurekebisha upungufu wa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa kuliko inavyotegemewa.Watu wengi wamejaribu kufanya hivyo na matokeo wamerudisha sifa na shukrani kwa somo hilo,tuwasiliane kwa maelezo zaidi.

HUONDOA SUMU MWILINI.
  Lycopene ipatikanayo ndani ya tunda hili husaidia kuzuia sumu mbalimbali mwilini zisiudhuru.Pia sumu zipatikanazo kwenye baadhi ya nyama (protini) hurekebishwa kwa kirutubisho hiki.Pia baadhi ya protini ngumu tunazokula kila siku husagwa nakufanywa nyepesi kuchukuliwa ndani ya mwili na kufanya kazi husika kuliko kutolewa nje kama uchafu/kinyesi.

HUSAIDIA MATATIZO YA CHOO NA UPUNGUFU WA MAJI.
 Kuwepo kwa maji kwa asilimia nyingi pamoja na kamba lishe,kunasaidia kurekebisha matatizo ya choo na kibofu cha mkojo.Kwa wenye magonjwa haya,kwa kutumia tunda la Tikiti-maji wataweza kuyatibu na kuyazuia na kwa wale ambao hawana wanashauriwa kutumia tund hili ili kujihakikishia ulinzi wa afya zao na wasisubiri mpaka wakutane nayo.

HUPUNGUZA SHINIKIZO LA DAMU KWA KIWANGO KIKUBWA.
 Utafiti uliofanywa na watu wamarekani ulibaini kuwa watu wengi walio na tatizo la shinikizo la damu (PRESURE) na wakatumia tunda hili katika milo yao waliweza kupunguza kasi ya tatizo hilo.
Hii inatokana na uwepo wa sukari asilia ambayo ni muhimu kurekebisha kiwango cha sukari mwilini na kukuleta kiwango sawa cha sukari inayohitajika.

MAGONJWA YA MENO NA MIFUPA. 
  Tikiti-maji lina madini kama vitamini C ambayo husaidia kuzuia magonjwa ya fizi pamoja na meno (KISEYEYE),hivyo ulaji wa tunda hili hasa kwa watoto utapunguza kasi ya athari za ugonjwa huu.
Watoto wengi pia hulipenda kutokana na sukari yake iliyomo ndani ya tunda hili hivyo haitakua vigumu mtoto kulila kwani kuna baadhi ya matunda ambayo sio rafiki kwa watoto na asilimia kubwa hayapendwi kutokana na uchachu,uchungu au kiwango kidogo cha sukari kinachopatikana.

HUIMARISHA UBONGO.
 Uwepo wa vitamini Bcomplex (B6) kwenye tunda hili husaidia kuimarisha kazi ya ubongo na kuufanya kuwa mchangamfu kwa muda mrefu.Baadhi ya matatizo yanayoyaukumba ubongo huweza kuzuiwa na kurekebishwa na vitamini hiyo.Unashauriwa kama wewe ni mwanafunzi utumie tunda hili kwa manufaa ya kuufanya ubongo wako kuwa active.Vilevile hata kwa wazee na walevi wanaokutana na matatizo ya kusahau watakuwa vizuri endapo watatumia tunda hili.Si kuimarisha tuu bali tunda hili hutumika kama lishe ya ubongo.


   Siyo ivyo tuu,licha ya kuchangia kwa kiasi kikubwa urekebishaji wa tatizo hilo tunda hili lina uwezo mkubwa sana wa kusaidia moyo kuweza kufanya kazi kwa kiwango sahihi na sio kuzidiwa na kazi.Hii husababisha kuupa moyo muda wa kutosha wa kupumzika kwa kufanya kazi kidogo.
  Unaweza aukatumia tunda hili kama juisi na pia ukala kama unavyokula matunda mengine ila vyote hufikisha virutubisho mwilini,lakini pia kwa matatizo mengine ambayo tumeyaona hapo juu unashauriwa kutengeneza juisi ya tunda hili bila kuondoa kitu chochote kile nikimaanisha kuanzia maganda mpaka mbegu zake.
      Anza mazoea sasa yakutumia matunda kama lishe mbadala na kinga dhidi ya magonjwa na usisubiri mpaka ukutane na magonjwa ndipo ukumbuke kuna lishe ya matunda,fanya hivyo kwa manufaa ya afya yako binafsi na sio kwa kulazimishwa wala kuiga ulaji wa mtu mwingne.
Ifahamike wazi kwamba ulaji wa matunda kiafya haukusababishii wewe usimwone daktari,bali kuna matatizo mengine ambayo ni lazima ukafanyiwe uchunguzi na ukatibiwe kwa mtaalamu wa afya kwani yanaweza kuwa ni zaidi ya ufikiriavyo.
 Kwa maoni,ushauri na mengineyo usisite kuwasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini. Ahsante

PHONE:  0673666791

Email: goldamplat@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni