Jumatano, 18 Januari 2017

FENESI.

   Kama ilivyo ada ni wasaha mwingine ambao tunamshukuru mungu kwa kutupa uzima na kukutana tena katika makala yetu ya kila siku.Tunapaswa kumshukuru mungu kwani bila yeye hakuna ambalo tunalifanya na kuwa sahihi
Leo nitakupeleka moja kwa moja kuona umuhimu wa tunda aina ya fenesi kiafya ya ndani na nje ya mwili.
 
    Tunda la fenesi ni moja kati ya matunda yenye sukari kwa kiasi chake,ulaji wa 100g za fenesi hukupa karolizi 90 kutokana sukari aina ya fructose na sucrose zilizomo ndani ya tunda hili.Kutokana na ukweli kwamba matunda mengi huwa na virutubisho vingi vinavyofanana hasa vitamini C,utaona kazi nyingi za baadhi ya matunda pia hufanana.Tuangalie faida za tunda hili kiafya kama ilivyo kawaida yetu:

MAGONJWA YA MOYO.
Sababu mojawapo ya magonjwa ya moyo ni pamoja na sukari kuwepo kwa wingi ndani ya mzunguko wa damu hii husababisha kuongezeka kwa kasi ya usafirishaji wa damu na mapigo ya moyo (blood pressure).Hii hupunguzwa kutokana na tunda la fenesi kuwa na kiwango cha sukari ambayo husaidia kurekebisha sukari mwilini.Hata hivyo mafuta yapatikanayo ndani ya fenesi hayana lehemu,hivyo ni mafuta sahii kutumika na yana uwezo mkubwa wa kukabiliana na tatizo la pressure hasa ya kupanda.
 
HUTIBU TATIZO LA DAMU.
Uwepo wa potasium na baadhi ya madini kama folic acid ndani ya tunda hili husaidia kwa kiasi kikubwa kusulihisha suala la damu.Kwa kuwa na anti oxidant Fenesi husaidia kuondoa sumu mwilini na kukupunguzia kasi ya magonjwa ya kansa na kulipunguzia ini kazi nzito ya kupambana na sumu mwilini.

MIFUPA NA MENO.
Mifupa huwa dhaifu kutokana na umri,vyakula tunavyokula pamoja na maradhi lakini vyote hivyo huweza kuepukika kama utaamua kuanza leo afya lishe na tunda hili.Fenesi lina madini mengi ya magnesium na kalisium ambayo husaidia kwa kiasi fulani katika kuimarisha mifupa.Hata magonjwa ya meno hutibiwa kwa fenesi kwani lina kiwango kikubwa cha vitamini Cambayo hufanya kazi nzuri katika kuimarisha uimara wa meno.
 
HULINDA NGOZI.
Dawa sahihi ya ngozi zilizojikunja (kama za wazee) ni Fenesi,hii ni kutokana na kiasi kikubwa cha mafuta ambacho tunda hili kinacho ambacho husaidia katika kulainisha ngozi na kuipa muonekano mwaroro.Sio hadithi za dhahania bali ni ukweli kwamba mafuta ya ngozi yatokanayo na fenesi ndio yaliyothibitishwa kuwa mafuta bora kwa afya ya ngozi ya binadamu.Fenesi huipa ngozi mwonekano kama wa ngozi ya mtoto mdogo,hivyo kwa akina dada si vyema sana kuhangaika na vipodozi vyenye madhara na gharama kubwa bali ubadilishe mazoea na kuanza kutumia fenesi kwa uzuri wa ngozi yako.
 
UNG"AAVU WA MBONI ZA MACHO.
Kutokana na uwepo wa vitamini A ambayo kazi yake kubwa ni kuyafanya macho yawe na uwezo mzuri wa kuona,pia hupatikana ndani ya tunda hili nakufanya kuwa na kazi muhimu ambayo inahitajika kila siku kwani tatizo la macho kwa kiasi kikubwa huathiri mwenendo mzima wa maisha yetu ya kila siku.
      Ulaji wowote uliopitiliza ni hatari kwa afya yako hata kama kitu hicho kitakua na faida mara mia,unatakiwa kula kistaarabu na kwa kiasi na sio kwamba umejua kuna faida za kutumia chakula hicho ukatumia zaidi.Mchanganyo wa fenesi na vyakula vingine huleta sumu ndani ya mwili wako,kaa na taadhari
 ONYO: USIJARIBU KULA FENESI NA KUNYWA SODA YA COCOA-COLA KWA MFUATANO.
 Kufanya hivyo unahatarisha maisha yako kwa muda mchache sana,kwani mchanganyiko huo husababisha utengenezwaji wa sumu ifananayo na nyoka aina ya cobra.
Utafitii uliofanyika china umedhihirisha jambo hilo:

 Kwa mapendekezo,maoni,maswali na ushauri wowote  juu ya tatizo lolote kuhusiana na AFYA usisite kuwasiliana nasi muda wowote.
PHONE:        0673666791


Jumanne, 17 Januari 2017

NANASI.

 

     Leo tena katika makala nyingine tunakutana kuzungumzia tunda aina ya nanasi,kabla ya kuanza mada yetu hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote aliyotutendea na kutuweka salama mpaka muda huu.Ni matumaini yangu ni wazima wa afya na mmejaaliwa kuiona siku nyingine hivyo sifa na utukufu arudishiwe Mungu muweza yote.
   Nanasi kama linavyojulikana kwa jina lingine la Pineapple ni tunda linalopendwa na watoto wengi kwani lina sukari nyingi ukilinganisha na matunda mengine.Licha ya watoto pia hata watu wazima wanapenda sana juisi ya nanasi kutokana na utamu wa ladha iliyokua nayo.Tunda hili ni miongoni mwa matunda yanayoongoza kutibu magonjwa ya koo na yamekuwa yakitumika na wengi kutokana na kazi hii.Baada ya kumenywa vizuri na kuwa tayari kwa kuliwa,nanasi halitakiwi kuhifadhiwa ndani ya friji kwani hupoteza ubora wa virutubisho vyake bali kwa kuliweka katika chombo chenye mfuniko na kulihifadhi vizuri hulipa thamani yake sahihi hata kwa muda wa zaidi ya siku nne.
   Kama yalivyo matunda mengine,nanasi linaweza kuliwa kama jinsi lilivyo au likatengenezewa juisi,njia zote ni sahihi katika kupata virutubisho sahihi vya tunda hili.Tuangalie umuhimu wake katika kutibu na kuzuia baadhi ya magonjwa;

MAGONJWA YA KOO.
 Tunda hili limeonekana kuweza kupambana na ugonjwa wa kuwashwa na kuvimba koo

MAGONJWA YA TUMBO.
 Udhaifu wa tumbo kushindwa kusaga chakula hasa protini hurekebishwa na tunda la nanasi.Hii ni kutokana na uwepo wa kimeng"enya cha aina ya Bromelain ambacho hufanya kazi kubwa ya kusaidia kusaga vyakula vilivyo na ugumu katika usagaji wake.Hii hupelekea tatizo hilo kutatuliwa na tunda hili hivyo kulifanya kuaminika na watu wengi katika kutatua tatizo hilo.

KULAINISHA CHOO.
 Kamba lishe zilizomo ndani ya papai husaidia tatizo la choo na kutoa choo laini na sio kigumu.Kwakua nanasi lina majimaji kwa kiasi kingi huweza kuzuia tatizo la uhaba wa maji katika mfumo wa chakula mwilini mwa binadamu.Kwa ushauri wa tatizo hili tumia nanasi na uone mafanikio sasa

HUONGEZA DAMU.
 Nanasi lina kiasi fulani cha madini chuma ambayo husaidia katika kuongeza damu kwani huusika na utengenezaji wa damu mwilini mwa binadamu.wagonjwa wengi waliopungukiwa na damu hushauriwa kutumia tunda hili kaam njia mbadala ya kuongeza damu mwilini mwao.
 

BARIDI YABISI (ATHRITIS).
 Baadhi ya magonjwa ya baridi yabisi yaani magonjwa ya jointi hutatuiliwa kwa ulaji wa nanasi kutokana na uwingi wa vitamini zilizomo kwenye tunda hili kama vile vitamini A,B, na C.Wazee wengi huwa na tatizo hili hivyo hushauriwa kutumia nanasi kwa kutatua tatizo hili.

     Uwepo wa vitamini hizo husaidia kukabiliana na magonjwa mengine kama ya fizi,meno na magonjwa mengine ya mifupa na sio magonjwa machache niliyoyaelezea hapo juu tuu bali na mengine ambayo tutazidi kuelezana kadri tunavyokua pamoja.

     Kuna dhana inayosikika kwamba nanasi si tunda bora kwa akina mama wajawazito kwani huwaletea matatizo,jambo hilo sio la kweli na ni kama hadithi zilizo simuliwa zamani za mababu zetu za kukataza mama mjamzito kutumia baadhi ya vyakula fulani.
Tumia nanasi ukiwa na lengo la kuboresha na kuimarisha afya yako na sio kwa mazoea ya kula ilimradi umekula.
   Fuata kanuni na taratibu sahihi za afya kwa matokeo sahihi ya afya bora na sio kufanya kwa mazoea,mfundishe mwanao,rafiki na hata jirani yako juu ya umuhimu wa tunda hili naye anufaike.
Kwa mtazamo na maoni yoyote juu ya jambo lolote lihusianalo na afya yako usisite kuwasiliana nasi kwa namba hapo chini,Ahsante.

  PHONE; 0673666791
  Email; goldamplat@mail.com

Jumatatu, 16 Januari 2017

MACHUNGWA


        Habari ndugu msomaji ni matumaini yangu u mzima wa afya na Mungu amekujal;ia afya iliyo imara,kama ni mgonjwa pia unatakiwa kumshukuru mungu na kuangalia wapi ulikosea kufuata kanuni za afya na ujirekebishe ili kurudia katika hali yako ya uzima.
Leo tutaangalia umuhimu wa tunda aina ya Chungwa kwani wengi wamekua wakiniuliza baadhi ya maswali kuhusiana na tunda hili.
    Kwanza kabisa tunda hili halitakiwi kuliwa na mtu mwenye vidonda vya tumbo kama hajala kitu chochote kwani ni aina ya tunda lenye asidi ambayo inaweza ikamletea matatizo katika vidonda vyake.Pia mbegu za tunda hili licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini,vitamini na madini mengine,zinz kiwango kikubwa cha sumu aina ya Cynide (sayanid) ambayo kama itapatikana kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu ni sumu ambayo inaweza kuua kwa haraka.
 Faida za virutubisho ambavyo vipo ndani ya chungwa hupatikana katika sehemu kuu mbili nazo ni Maji ya chungwa (mchuzi wa chungwa) na kwenye nyama ya chungwa.Unashauriwa kula chungwa lote na sio kukamua maji yake na kisha kulitupa kwani utakosa kambalishe zipatikanazo kwenye nyama ya chungwa.Watoto wadogo hufanya hivyo mara nyingi,sio inamaanisha wanakosa virutubisho vyote hapana! bali wanapata vichache vile vilivyomo ndani ya mchuzi pekee.
 Hivyo na kwa wewe ambae ulikua huafahamu jambo hilo sasa umelifahamu na nina imani utabadilika na kulifanyia kazi kwa manufaa ya afya yako mwenyewe.
   Hata hivyo licha ya yote hayo bado tunaona tunda hili lina faida mbalimbali mwilini kama vile;

UKOSEFU WA CHOO.
 Uwepo wa kambalishe ndani ya tunda hili husaidia katika usagaji wa chakula na kuondoa kabisa tatizo la choo.Pia kolesto zilizopo mwilini hupungua kwani umuhimu wa kambalishe hizi huonekana katika usagaji wa chakula na kusababisha mafuta yote yaliyozidi mwilini kutumika kwa kuyeyushwa na hivyo kufanya tatizo hili lisiwepo kabisa.
 
MAGONJWA YA MOYO.
 Flavonoidi pamoja na vitamini C inatopatikana ndani ya tunda hili husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kama vile mafuta kujaa ndani ya mishipa ya moyo kama tulivyoona hapo juu.
 
MAGONJWA YA MENO NA FIZI.
 Uwepo wa vitamini C ambayo husaidia katika kupambana na magonjwa ya udhaifu wa meno na fizi,utakusaidia katika kuimarisha afya ya meno na fizi zako kwa ujumla.

MAGONJWA YA MAPAFU.
 Chungwa lina kiasi kikubwa cha vitamini B6 na madini ya chuma ambayo husaidia katika utengenezaji wa seli nyekundu za damu ambazo huusika na usafirishaji wa hewa safi mwilini.Hii huondoa matatizo ya mapafu na mzunguko wa hewa safi mwilini moja kwa moja.

SHINIKIZO LA DAMU.
 Machungwa ni muhimu kwa wagonjwa wenye shinikizo kubwa la damu (presha) kwani kwa kuondoa mafuta yaliyorundikana kwanye mishipa ya damu pamoja na kuwa na virutubisho vya magnesium huondoa kabisa tatizo hili na kufanya mwenye tatizo kama hilo kupona na kujisikia vyema.
   Si mpaka uwe mgonjwa ndio uanze kutumia machungwa na matunda mengine bali kinga ni bora kuliko tiba.Ni bora kujiwekea mazoea ya kula matunda kwa wingi ili kupata virutubisho vinavyohitajika vikawe kama akiba ya baadae na kinga kwa magonjwa nyemelezi.

MAGONJWA YA FIGO.
 Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kurekebisha Ph ambayo itakufanya uwe na hali iliyo timilifu ndani ya mwili wako hii hulipumzisha ini pamoja na figo katika kufanya kazi nzito ya kurekebisha na kupambana na hali inayobadilika mara kwa mara.
 
KUONDOA CHOLESTEROL.
 Uwepo wa kirutubisho cha lemonin ndani ya machungwa husaidia kwa kiasi kikubwa sana kuondoa mafuta ambayo hayahitajiki ndani ya miili yetu.Hasahasa kwa watu wanene kupita kiasi (obese) wanaweza wakapunguza unene huo kwa kufuata utaratibu wa matumizi bora na sahihi ya matunda kama machungwa na mengineyo.

   Ulaji wa chungwa pia umetofautiana kama tulivyoona hapo juu,hivyo unaweza ukaamua wewe utumie tunda hili kama juisi au kama tunda la kawaida kulila.Na pia ulaji wake tumeuangalia hapo juu hivyo nakushauri uache kula kwa mazoea, na uanze kula kwa faida ya afya na sio ladha pekee.
Kwa ushauri na tatizo lolote linalohusiana na afya yako usisite kuwasiliana nasi muda wowote na pia kama una maoni,ushauri na vyovyote uonavyo wewe wasilisha kwa mawasiliano yetu hapo chini.Mungu akubariki.

    PHONE: 0673666791

    Email: goldamplat@mail.com

                www.amplatblogspot.com

Ijumaa, 13 Januari 2017

EMBE
Uhali gani ndugu msomaji wa makala haya,ni matumaini yangu u mzima wa afya na mugu amekujalia kuamka salama hivyo tunapaswa kumshukuru kwa neema hii.Twende moja kwa moja kwenye mada yetu ya leo inayohusiana na tunda aina ya embe.


Katika matunda yenye sukari ni pamoja na tunda hili,ukiachilia mbali ndizi,nanasi na mapera.wengi wetu hupenda kulitumia tunda hili kama kutengenezea juisi,kulila likiwa limeiva au bichi na hata bidhaa za vindani kama vile achali na mango pickle.Wote huu ni ulaji ambao unaongeza virutubisho mwilini vilivyo katika embe.Faida nyingi huonekana katika ulaji wa embe na sio tuu nyama yake bali hata miziz,majani pamoja na maua yake pia,tuone baadhi.
MAGONJWA YA MACHO.
Embe lina vitamini A kwa kiwango kikubwa baada ya karoti ukilinganisha na matunda mengine,uwezo huu husaidia kudhibiti magonjwa ya ukavu macho na udhaifu mwingine wa macho.tumia embe kwa lengo la kutibu macho yako na sio kwa mazoea ya kula kwa kujifurahisha.

UDHAIFU WA TAYA NA MENO.
Uwepo wa vitamini C katika tunda hili,unahakikisha kazi ya uimarishaji wa meno na taya/fizi za meno.Kwani vitamini C huzuia ugonjwa wa udhaifu wa meno (scurvy).kula embe kawaida unaweza kulila likiwa lenyewe au ukatengeneza juisi ya tunda hili.

MALARIA SUGU.
Majani machanga ya mti wa muembe hutumika kama kinga na tiba ya malaria sugu kwa asilimia kubwa.Unaweza kuyatumia kwa kuyatafuna baada ya kuyaosha vizuri au pia unaweza kuyachemsha na kuyaacha yapoe kwa muda ndipo uyatumie maji na majani yenyewe.
NB: Katika kutibu ugonjwa huu hakikisha unakula majani haya machanga kwani yana nguvu kubwa ya kupambana na wadudu wa malaria sugu.

PUMU.
Majani ya muembe yakikaushwa vizuri katika kivuli (ili kuzuia alkadosisi kupotea) na kusagwa pia hutumika katika kutibu tatizo la pumu.Hii imewasaidia wengi katika kufanya ivyo na wameondokana na tatizo hilo.Saga majani hayo na uchanganye na maji kisha uyatumie kwa kunywa utapata matokeo.

MATATIZO YA UZAZI.
Tunda hili lina kokwa ambalo ndio dawa kubwa ya tatizo la kuziba mirija ya uzazi na tatizo hili haliwapati akina mama tuu bali hata kwa akina baba nao hukumbwa nalo.Chukua kokwa likaushe vizuri na ulisage ili kupata unga wake,halafu tumia unga huo kuchanganya na maji kisha kunywa hayo maji angalau glasi moja kabla ya mlo wako wowote ule.

Matatizo mengine kama ufinyu wa utoaji maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha huondolewa kwa kutumia maua ya maembe,pia hata harufu mbaya ya mdomo huondolewa kwa matumizi ya majani ya maembe.
Utumiaji wa tunda hili kama dawa utaona mabadiliko yake ndani ya muda mfupi kama ukizingatia utaratibu wa lishe kiafya na sio kwa mzoea.
Nikushukuru kwa muda wako wa kusoma na nikuombe uanze kufanyia kazi kama kweli unataka mabadiliko kiafya na si uchukulie kawaida kama ulivyozoea.
Kwa ushauri,maoni na matatizo yoyote yahusuyo afya yako,usisite kuwasiliana nasi kwa;

Phone; 0673666791
Email; goldamplat@gmail.com amplat afya kwanza

Jumatano, 11 Januari 2017

 PAPAI


Habari za muda huu ndugu msomaji,naamini u mzima wa afya na furaha hivyo huna budi kumshukuru Mungu.Kwa wale walio na matatizo ya kiafya na kiakili nao hawana budi kumshukuru mungu kwani pumzi waliyopewa kwa siku ya leo inatosha kabisa kusema asante kwa Mungu wako.
   Leo tutaangalia umuhimu wa tunda la aina nyingine,ambalo ni papai.tunda hili pia sio geni na linafahamika na idadi kubwa ya watu nchini kwetu.Lichz ya kuwa watu wengine hula tunda hili kutokana na utamu wa sukari iliyomo ndani mwake,lakini ukweli kwamba tunda hili lina virutubisho vingi ambavyo vitakufafanya uwe na afya bora na uondokane na magonjwa mbalimbali,tuanze kuangalia tatizo moja baada ya lingine.

USAGAJI WA CHAKULA MWILINI.
 Watu wengi wanaopata choo kigumu ni wavivu wa kunywa maji,labda hawaoni umuhimu wake au wana mazoea ya kunywa maji pale wasikiapo kiu tuu.Utaratibu huu sio mzuri ingawa umezoeleka na watu wengi hivyio ni lazima tupingane nao.Kutokana na ulaini wa papai na kimeng"enya cha PAPAIN kilichopo ndani ya tunda hili,husaidia kulainisha chakula tumboni na kukifanya kiweze kusagika kwa urahisi zaidi.Ili uondokane na tatizo la usagaji wa chakula na magonjwa mengine yahusikayo na hayo,huna budi kutumia papai na kujizoesha kunywa maji mara nyingi uwezavyo kwa siku.Si tuu kwa ajili ya tatizo hili bali na matatizo mengine pia.


MAGONJWA YA UKOSEFU WA VITAMINI.
 Katika matunda yenye utajiri wa vitamini,papai ni mojawapo katika orodha kwani lina vitamini A,B,C,D na E.vitamini zote hizo hutumika kurekebisha magonjwa kama ukavu macho,kiseyeye na matege (kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5).Vilevile magonjwa mengine ambayo sijayataja hapo juu yatokanayo na ukosefu wa vitamini hizo huzuiliiwa kwa kula papai kwani litasababisha uwepo wa vitamini hizo na kuzuia magonjwa hayo kutokea.

UPONYAJI WA VIDONDA.
 Ute ute/Maziwa ya papai hutumika kutibu vidonda vya aina zote,kuanzia vidonda vya ndani ya mwili hata vile vya nje ya mwili wa binadamu.Vidonda kama vya tumbo huweza kutibiwa kwa maziwa hayo yatokanayo na papai vile vile hata vidonda vya nje kama kuungua na kuumia sehemu fulani ya mwili hutibiwa kwa kupaka mafuta hayo sehemu iliyoathirika/yenye jeraha.
 

MAGONJWA YA INI NA FIGO.
 Ini ndio ogani pekee ambayo hupambana na sumu mwilini mwa binadamu,ukiachilia mbali figo ambayo kwa kiasi fulani huondoa sumu.Mbegu za papai hulipa ini nguvu za kuendelea kupambana na sumu ziingiazo mwilini mwetu na kukupunguzia kiwango kikubwa cha sumu ambazo zitaathiri afya yako.Pia majani ya mpapapi yakichemshwa kwa dakika 15 na kuutumiwa kwa kunywa angalau lita 1.5 kwa siku,husafisha kabisa figo na kuondoa matatizo yatokanayo na mfumo wa utoaji taka mwili (mfumo wa mkojo)

MAGONJWA YA MAPAFU.
  Kwa watumiaji wa sigara na wale wote wanaokumbana na adha za moshi kila kukicha,utumiaji wa papai utakupunguzia madhara ya moshi kwa asilimia kubwa (zaidi ya 80%).Kutokana na vitamini A iliyopo kwa wingi ndani ya tunda hili madhara yatokanayo na moshi huzuilika,kwani tunajua wazi kwamba moshi huathiri mfumo wa upumuaji wetu kwani ni hewa mbaya ambayo inaingia mwilini (kwenye mapafu) na kuingilia mfumo mzima wa upumuaji.
Wagonjwa wa macho pia nawashauri kutumia papai kama dawa na sio kama mlo wa mazoea tena,kwani kwa kufanya hivyo utajihakikishia usalama na uhai wa afya yako.
 Kwa ushauri na matatizo yanayohusu afya yako,wasiliana nasi muda wowote upate ushauri.Pia tunakaribisha maoni,mapendekezo na mitazamo mbalimbali.

Contact: 0673666791
Email: goldamplat@mail.com

Jumapili, 8 Januari 2017


       TANGO

Image result for faida za tango kiafyaImage result for faida za tango kiafya

Habari za tangu tulipokuwa pamoja muda uliopita,ni matumaini yangu ni wazima wa afya na hatuna budi kumshukuru mwanyezi mungu.Kwa wale walio wagonjwa na hawajiwezi mungu awasaidie na niwape pole pia.
Tuanze na mada yetu muhimu ya kutambua umuhimu wa virutubisho vipatikanavyo ndani ya matunda.Tuanze na umuhimu wa Tango,kama tunavyolifahamu tunda hili ni muhimu kwa afya kwani lina kazi nyingi sana katika miili yetu.maganda yake na mbegu zake ndio huwa na umuhimu mkubwa kama tutakavyoona.




Tunapoongelea umuhimu wa tango tunaona uwezo wake mkubwa katika kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali kama vile;

MAGONJWA YA NGOZI.
Tango hujulikana kwa kuwa na maji mengi ambayo husaidia kulainisha ngozi,tangu zamani tunda hili lilitumika katika kutibu magonjwa ya ngozi.Weusi upatikanao kuzunguka maeneo ya macho,huweza kuondolewa kwa kutumia vipande kadhaa vya tango.Chukua vipande viwili vya tango na usugulie kuzunguka eneo lenye weusi,kwa kufanya hivyo utaweza kutibu eneo hilo.

HARUFU MBAYA MDOMONI.
Kama kinywa chako kinatoa harufu mbaya na unashindwa kuzuia,unaruhusiwa kutumia kipande kimoja hadi viwili kwa kutafuna.Kwa kufanya hivyo utazuia harufu mbaya mdomoni.

KUONGEZA UTE KWENE JOINTI.
Ifahamike kwamba maji yapatikanayo kwenye tango husaidia pia katika kuongeza uteute katika joint za mwilini.Hii huzuia mifupa kusagana na hivyo matatizo ya mifupa kushughulikiwa ipasavyo.kula tango kwa lengo la kutibu matatizo na sio kwa mazoea.

  Faida nyingine za tango ni kama vile,kusafisha kiatu cha rangi nyeusi na kufanya king"ae zaidi.Tango lina vitamini B1,B2,B3,B4,B6 na B12 pia lina kashiumu na potashium kwa wingi.
    

Ijumaa, 6 Januari 2017

PARACHIHI.


Habari za muda na wakati mwingine tena ndugu msomaji,ni matumaini yangu u mzima wa afya na Mungu anakujalia katika mambo unayoyafanya kila siku hivyo huna budi kumshukuru.Katika kipindi kilichopita tuliona umuhimu wa tunda aina ya ndizi,na leo tutaangalia umuhimu wa tnda lingine aina ya parachihichi.
   Katika utafiti mmoja uliofanywa huko marekani ulionyesha kuwa watu wanaokula parachichi huwa na afya bora na wenye kunawili na kung"aa kwa ngozi zao ikilinganishwa na watu ambao hawatumii tunda hili.Kutokana utofauti na matunda mengine,parachichi linapendwa sana watoto wadogo kwani ni rahisi kulimeza.Hii inatokana na uwingi wa mafuta yapatikanayo ndani ya tunda hili ukilinganisha na matunda mengine yenye uwingi wa wanga pamoja na vitamini.tunda hili pia lina kiasi kikubwa sana cha madini ya aina ya potashium,fosforasi na magineziamu,bila kusahau vitamini zilizopo humu kama vile vitamini A,E na C.Tuangalie umuhimu wa parachichi kiafya.

    MAGONJWA YA MOYO NA SHINIKIZO LA DAMU.
Magonjwa ya moyo mara nyingi hutokana na mtindo wa maisha na vyakula tunavyokula kila siku,mafuta mengi tunayotumia huongeza kiasi kikubwa cha LEHAMU mwilini hupelekea kujirundika ndani ya mishipa ya damu na kusababisha presure za kupanda na kushuka.Kwakuwa parachchi lina mafuta mengi yasiyokua na lehamu,hivyo nibora litumike kama mbadala wa kupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini.

    KUPUNGUZA UZITO WA MWILI.
Kwa kula sana parachichi husaidia mwili katika kazi yake ya kumeng"enya chakula vizuri na kuzuia urundikanaji mwingi wa vyakula visivyokua na kazi mwilini.kama tulivyoona hapo juu utumiaji wa mafuta yatkanayo na parachichi huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa mafuta yaletayo lehamu na kuongeza mafuta yasiyo na lehamu.Hii hufanya mwili kujisikia mwepesi muda wote.Parachichi ina kiwango kikubwa cha kirutubisho cha fiba(nyuzinyuzi) ambacho huwa hakimeng"enywi tumboni lakini kikiwa na umuhimu mkubwa katika kusaidia kupata choo kizuri.

    AFYA YA NGOZI.
Tunafahamu kwamba ngozi ya binadamu huwa ina mafuta yake asili,bila kupaka mafuta ya kawaida hakumaanishi ngozi itakauka kabisa.ulaji wa parachichi huchangia ongezeko la mafuta asilia ndani ya mwili na kufanya ngozi kupata mafuta mengi ambayo hutumika kujilainisha kila itakapokauka.mafuta haya huipa ngozi muonekano mzuri na wenye afya.
Mbadala wa kula,mafuta yapatikanayo ndani ya parachichi huweza kupakwa katika ngozi kwa njia ya asili na mtu akajisikia murua.

    LISHE BORA KWA WALE WENYE KISUKARI.
Faida moja wapo ya chakula kutojirundika mwilini ni pamoja na kupunguza mrundikano wa sukari nyngi mwilini.Fiba ipatikanayo kwenye tunda hili husaidia mmeng"enyo wa chakula na kupunguza mrundikano wa sukari mwilini.Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari na pia uwepo wa mafuta yake huchangia ufanyaji kazi mzuri wa homoni aina ya insulini katika urekebishaji wa sukari mwilini.

    MATATIZO YA UZAZI.
Ni dhahiri kwamba mtu mwenye matatizo ya moyo hukumbwa na matatizo ya uzazi pia,hii hutokana na kufanana kwa visababishi vya matatizo haya kwa namna moja ama nyngine.Hivyo unashauriwa kutumia tunda hili kwa kurekebisha na kuepuka sababu hizo.
Parachichi limeonyesha kuwa na faida kubwa katika kuboresha afya ya macho kwa uwepo wa vitamin A na vitamini nyingnezo kama vile E na C,pia husaidia kulainisha viungo vya mwili na kukufanya uwe mkakamavu muda wote kwani mafuta yapatikanayo kwenye tunda hili huongeza utepe kwenye jointi na kufanya mifupa kujongea vyema.Parachichi hutoa matokeo mazuri endapo litatumiwa kwa kufuata kanuni na taratibu husika za lishe.

   Usisite kuwasiliana nasi kwa ushauri,tiba na mapendekezo yoyote juu ya afya yako.
Wasiliana nasi kwa;

  Phone: 0673666791