Ijumaa, 6 Januari 2017

PARACHIHI.


Habari za muda na wakati mwingine tena ndugu msomaji,ni matumaini yangu u mzima wa afya na Mungu anakujalia katika mambo unayoyafanya kila siku hivyo huna budi kumshukuru.Katika kipindi kilichopita tuliona umuhimu wa tunda aina ya ndizi,na leo tutaangalia umuhimu wa tnda lingine aina ya parachihichi.
   Katika utafiti mmoja uliofanywa huko marekani ulionyesha kuwa watu wanaokula parachichi huwa na afya bora na wenye kunawili na kung"aa kwa ngozi zao ikilinganishwa na watu ambao hawatumii tunda hili.Kutokana utofauti na matunda mengine,parachichi linapendwa sana watoto wadogo kwani ni rahisi kulimeza.Hii inatokana na uwingi wa mafuta yapatikanayo ndani ya tunda hili ukilinganisha na matunda mengine yenye uwingi wa wanga pamoja na vitamini.tunda hili pia lina kiasi kikubwa sana cha madini ya aina ya potashium,fosforasi na magineziamu,bila kusahau vitamini zilizopo humu kama vile vitamini A,E na C.Tuangalie umuhimu wa parachichi kiafya.

    MAGONJWA YA MOYO NA SHINIKIZO LA DAMU.
Magonjwa ya moyo mara nyingi hutokana na mtindo wa maisha na vyakula tunavyokula kila siku,mafuta mengi tunayotumia huongeza kiasi kikubwa cha LEHAMU mwilini hupelekea kujirundika ndani ya mishipa ya damu na kusababisha presure za kupanda na kushuka.Kwakuwa parachchi lina mafuta mengi yasiyokua na lehamu,hivyo nibora litumike kama mbadala wa kupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini.

    KUPUNGUZA UZITO WA MWILI.
Kwa kula sana parachichi husaidia mwili katika kazi yake ya kumeng"enya chakula vizuri na kuzuia urundikanaji mwingi wa vyakula visivyokua na kazi mwilini.kama tulivyoona hapo juu utumiaji wa mafuta yatkanayo na parachichi huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa mafuta yaletayo lehamu na kuongeza mafuta yasiyo na lehamu.Hii hufanya mwili kujisikia mwepesi muda wote.Parachichi ina kiwango kikubwa cha kirutubisho cha fiba(nyuzinyuzi) ambacho huwa hakimeng"enywi tumboni lakini kikiwa na umuhimu mkubwa katika kusaidia kupata choo kizuri.

    AFYA YA NGOZI.
Tunafahamu kwamba ngozi ya binadamu huwa ina mafuta yake asili,bila kupaka mafuta ya kawaida hakumaanishi ngozi itakauka kabisa.ulaji wa parachichi huchangia ongezeko la mafuta asilia ndani ya mwili na kufanya ngozi kupata mafuta mengi ambayo hutumika kujilainisha kila itakapokauka.mafuta haya huipa ngozi muonekano mzuri na wenye afya.
Mbadala wa kula,mafuta yapatikanayo ndani ya parachichi huweza kupakwa katika ngozi kwa njia ya asili na mtu akajisikia murua.

    LISHE BORA KWA WALE WENYE KISUKARI.
Faida moja wapo ya chakula kutojirundika mwilini ni pamoja na kupunguza mrundikano wa sukari nyngi mwilini.Fiba ipatikanayo kwenye tunda hili husaidia mmeng"enyo wa chakula na kupunguza mrundikano wa sukari mwilini.Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari na pia uwepo wa mafuta yake huchangia ufanyaji kazi mzuri wa homoni aina ya insulini katika urekebishaji wa sukari mwilini.

    MATATIZO YA UZAZI.
Ni dhahiri kwamba mtu mwenye matatizo ya moyo hukumbwa na matatizo ya uzazi pia,hii hutokana na kufanana kwa visababishi vya matatizo haya kwa namna moja ama nyngine.Hivyo unashauriwa kutumia tunda hili kwa kurekebisha na kuepuka sababu hizo.
Parachichi limeonyesha kuwa na faida kubwa katika kuboresha afya ya macho kwa uwepo wa vitamin A na vitamini nyingnezo kama vile E na C,pia husaidia kulainisha viungo vya mwili na kukufanya uwe mkakamavu muda wote kwani mafuta yapatikanayo kwenye tunda hili huongeza utepe kwenye jointi na kufanya mifupa kujongea vyema.Parachichi hutoa matokeo mazuri endapo litatumiwa kwa kufuata kanuni na taratibu husika za lishe.

   Usisite kuwasiliana nasi kwa ushauri,tiba na mapendekezo yoyote juu ya afya yako.
Wasiliana nasi kwa;

  Phone: 0673666791


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni