Jumanne, 3 Januari 2017

   Habari za muda huu ndugu msomaji,ni matumaini yangu u mzima wa afya na furaha.Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa hali kama hii,pia kama ni mgonjwa na una matatizo ya afya unapaswa kumshukuru Mungu pia.
Pole kwa wenye matatizo mbalimbali nawasihi msikate tamaa bali endelea kujituma ili ukabiliane nalo,kwani changamoto zinakuinua na kukukfikish sehemu fulani
     Lengo langu leo nataka kukupa jambo muhimu katika maisha yako ambapo ukilielewa na kulifuata vizuri utaishi kwa furaha,amani na pasipo kupatwa na maradhi kwa muda mrefu.
     TUNAKULA ILI TUISHI na sio TUNAISHI ILI TULE,hivyo basi unatakiwa kuangalia ni nini unakula kitakachokufanya uishi salama.Siku zote chakula unachokula ndicho kinachoamua uendelee kuishi kwa muda gani.Tazama kuna mifano mingi ya watu walioishi zamani ambao walifuata kanuni na taratibu za milo sahihi na wakaishi muda mrefu,hata uzee ulipowafikia uliwakuta wakiwa nguvu zao.Mtindo wa maisha wa sasa umebadilika sana ukilinganisha na wa zamani,kwani kuna utofauti mkubwa kati ya watu walioishi miaka ya zamani na tunaoishi miaka ya sasa.Kuanzia kwenye kufikiri,kutenda kazi na muda wa kuishi vyote vimebadilika sana,hii imetokana na mtindo wa maisha ambao tumechagua kuishi ambao ni tofauti sana na ule wa zamani.
Sababu kubwa ambayo tutajifunza ni CHAKULA kwani imechukua asilimia kubwa ya maisha yetu.
     Ili uweze kuwa na afya bora ni lazima upate chakula bora,namaanisha chakula safi,kilichokamilika kwa kila virutubishio.Ni vizuri zaidi kupata chakula asilia kwani kina uhakika mwingi wa virutubisho asilia,pia sio vibaya kutumia vyakula vilivyoongezewa virutubisho.Naomba nieleweke kitu kimoja hapa naongelea vyakula vilivyoongezewa virutubisho na siyo vilivyoongezewa rangi,ladha au sukari.Ninaposema virutubisho namaanisha ni vile vitu ambavyo mwili unahitaji kwaajili ya kujijenga vizuri kwa kupambana na magonjwa,kukua na kuimarika.Unapopata chakula bora unajihakikishia usalama wa maisha yako na kujiongezea muda mrefu wa kuishi bila tatizo la kiafya,hii itatokana na kufuata kanuni za afya ambazo utazipata kupitia ukurasa huu,hivyo nakusihi fuatana na mimi ili tujulishane na kuelekezana vitu mbalimbali vinavyohusu afya zetu kwa ujumla.
    Jiandae kujua mambo mbalimbali yanayokuhusu kwa namna moja au nyingine,au kama sio wewe hata ndugu na marafiki zako ili ukitoka hapa ukawaelekeze nn wanatakiwa kufanya ili wawe na afya bora na waishi miaka mingi kama wakifuata taratibu za afya.
Nitakaribisha maswali,maoni,ushauri na mtazamo wako,pia kwa ww ambaye utakua na tatizo la kiafya na unahitaji kusaidiwa kwa tiba usisite tuwasiliane kwa njia hapo chini.
Mungu awabariki,tukutane wakati ujao:
Phone: 0673666791
Email: goldamplat@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni