Alhamisi, 5 Januari 2017

                Unaendeleaje ndugu msomaji wa AFYA KWANZA? Ni matumaini yangu nyote ni wazima wa afya.Tuchukue nafasi hii kumshukuru mungu kwa kutupa uhai na kutufanya kuendelea kuishi mpaka sasa.
Leo tuanze moja kwa moja na somo letu ambalo linahusiana na tunda mojawapo katika matunda ya hapo juu

NDIZI
Wengi tunalifahamu tunda hili na sio geni katika macho yetu,lakini linaweza likaw ni geni katika ufahamu wetu kutokana na kazi nyingi linazofanya tunda hili katika ujenzi na ulinzi wa afya yetu.Je tunafahamu kwamba ulaji wa ndizi mbivu mbili zitakuwezesha kufanya kazi kwa dakika 90 mfululizo?
      Kutokana na utafiti uliofanywa na taasisi ya afya nchini marekani,umebaini uwezo huo wa tunda la ndizi,(www.medical.news).
Ndizi ina aina fulani ya protini ijulikanayo kwa jina la TRYPTOPHAN ambayo hubadilishwa na kuwa SEROTON ambayo humfanya mtu ajisikie raha na amani ya akili hata kama ametoka kwenye msomgo wa mawazo.Tunashauri mtu kuacha kutumia vidonge vya kupunguza uchovu,pombe na hata sigara ili kujipa faraja na mapumziko ya akili lakini badala yake utumie tunda hili.

   MAUMIVU YA VIDONDA VYA TUMBO.

Ndizi huzuia maumivu yatokanayo na vidonda vya tumbo kwani hupunguza kasi ya uharibifu wa ukuta wa tumbo na tindikali inayozalishwa tumboni.

      SHINIKIZO LA DAMU.

 Ndizi pia husaidia kuweka sawa kiwango cha damu kwa kuongeza madini ya chuma pia husaidia kuweka sawa kiwango cha sukari kweny damu.hii hulifanya tunda hili kuwa na kazi ya kuratibu shinikizo la damu.Vilevile ndizi hutibu magonjwa ya figo na unashauriwa kutumia ndizi angalau moja kwenye milo yako kwa siku.Kwa uwezo huu wa ndizi,tunda hili linaweza kuwa moja ya dawa za kuzuia kama sio kuponya kabisa matatizo ya damu (anaemia).Wakina mama wengi wanashauriw kutumia ndizi kwani wanakutana na tatizo la upungufu wa damu mara nyingi.
    
   UWEZO WA KUFIKIRI.

Ndizi imekua ikiaminika sana katika kuongeza uwezo wa kufikiri baada ya jaribio kufanywa katika shule ya TWICKENHAM huko nchini uingereza,ambapo wanafunzi wapatao 200 walifanya tunda hili kuwa kama chakula cha mchana kwa muda upatao siku 40.Baada ya kufanya mitihani ikabainika kuwa wanafunzi hao ndio waliofaulu sana tofauti na wanafunzi wengine ambao hawakula ndizi.
Hii inatokana na ukweli kwamba,kuwepo na madini mengi ya aina ya potasium ndani ya tunda hili hufanya uwezo wa kufikiri kuamka na mwanafunzi kuchangamka.

   HANGOVER.

Ndizi huaminika sana kwa uwezo wake wa kuondoa uchovu utokanao na pombe ya jana,hii hutokana na uwezo wake wa kutuliza tumbo na mishipa ya fahamu.Juice ya mchanganyiko wa ndizi,asali pamoja na maziwa hufanya kazi hii.Tunashauri mtu kutumia glasi moja ya juisi hii ili kukata uchovu huo.
    Mbali na magonjwa hayo,ndizi pia imeaminika kutibu magonjwa mbalimbali kama vile mapigo ya moyo,kuondoa wasiwasi na magonjwa yatokanayo na upungufu wa protini.
Ndizi ikilinganishwa na matunda mengine huonekana kuwa na uwingi wa madini ya chuma na vitamini kwa wingi,pia inayo protini ya kutosha kuratibu mfumo mzuri ndani ya mwili.
  Fuata utaratibu mzuri wa ulaji wa ndizi ili uweze kupata matokeo bora ya afya yako.Tukutane muda na wakati mwingine Mungu akipenda.
Kwa ushauri na maoni wasiliana nasi kwa:
phone: 0673666791

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni