Jumatano, 4 Januari 2017

Habari za muda huu ndugu msomaji,naamini u mzima wa afya na furaha hivyo huna budi kumshukuru Mungu.Kwa wale walio na matatizo ya kiafya na kiakili nao hawana budi kumshukuru mungu kwani pumzi waliyopewa kwa siku ya leo inatosha kabisa kusema asante kwa Mungu wako.
          Tuanze makala yetu kwa kuangalia virutubisho vinavyohitajika na mwili ili kuweza kukua na kustawi vizuri.Kama utakumbuka vizuri katika makala iliyopita nilishauri matumizi ya virutubisho asilia(natural) na siyo vya kutengenezwa(artificial).Virutubisho hivi ni muhimu kutumika kwani havina nyongeza ya kitu chochote ambacho kitatishia afya yako tofauti na virutubisho vya kutengenezwa ambavyo huwa na nyongeza ya vitu mbalimbali kama vle sukari,chumvi,rangi pamoja na dawa za kuhifadhia virutubisho hivyo.
Mwili wa binadamu yoyote unahitaji WANGA(carbohydrate) kwaajili ya kuupa nguvu zitakazo muwezesha kufanya jambo lolote,unahitaji PROTINI (protein) kwaajili ya kukua,unahitaji pia VITAMINI(vitamins) kama virutubisho vya kuchangia shughuli mbalimbali ndani ya mwili.Tusisahau pia mwili unahitaji FATI/MAFUTA(fatty/lipids) kwaajili ya kukinga viungo vya ndani(organs) na baridi pamoja na kuzalisha joto.
       Tutazungumzia umuhimu wa vitu vyote hapo juu kila tutakapokutana na kwaleo tuanze na virutubisho aina ya VITAMINI.
Tunaposema vitamini tunamaanisha ni aina mojawapo ya virutubisho ambavyo mwili huitaji kwaajili ya kufanya kazi mbalimbali,kwamfano ili mwili uweze kutengeneza seli hai mpya ni lazima ipate virutubisho vitakavyofanya kazi ya kuanzisha zoezi hilo.
Vitamini hupatikana katika vyakula tunavyokula kila siku,ndio maana tangu mwanzo tuliona kuna umuhimu wa kula CHAKULA BORA na sio BORA CHAKULA.Utakapokula chakula kilichokamilika chenye virutubisho vyote utajihakikishia afya iliyo imara na hautakua na hofu ya magonjwa nyemelezi.
        Vitamini hupatikana sana katika matunda na mbogamboga,hii inatuonyesha umuhimu wa ulaji wa matunda na mbogamboga za majani ili kuvipata virutubisho hivyo.Tumshukuru Mungu ndani ya nchi yetu Tanzania tumepata neema ya kuwa na matunda ya aina mbalimbali pamoja na mboga za majani.Pia tuipongeze serikali yetu kwa kuhamasisha kilimo sio cha mazao ya nafaka,pia hata kilimo cha matunda na mbogamboga.Hii inaonyesha uelewa wa viongozi wetu katika kuwajali watu wake pamoja na afya zao.
        Matunda yapo ya aina mbalimbali kama vile NDIZI,MAPAPAI,MACHUNGWA,MAEMBE nk....na kila aina ya matunda hutofautiana na aina ya vitamini zilizopo ndani yake.
Kutokana na kanuni za afya matunda ni kitu muhimu sana na inashauriwa kula matunda kwenye kila mlo kwa siku nzima.Ni vyema kula matunda kabla ya chakula na pia ni vyema kula matunda kama kifungua kinywa chako mara baada ya kuamka.KWANINI?
Kanuni hizo mbili za tulizoziona hapo juu zina umuhimu wake mkubwa katika afya yako,tutakuja kuziona kipindi kijacho kama Mungu akipenda iwe ivyo
Nikutakie siku njema katika kufuata kanuni za afya yako ili uepuke magonjwa nyemelezi.
Kwa ushauri,maonina mapendekezo usisite kuwasilina nasi kwa njia hapo chini,muda wowote na saa yoyote,tupo kwaajili ya kusaidia.

Wasiliana nasi kwa;
    Phone: 0673666791
    Email: goldamplat@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni